dev.kisakuzi.com yashinda tuzo mbili mashindano ya blog Tanzania


Moja ya cheti cha ushindi ambacho dev.kisakuzi.com imekabidhiwa baada ya ushindi.

WEBSITE ya kimataifa ya Thehabari (dev.kisakuzi.com) imeshinda tuzo mbili katika mashindano yalioendeshwa na taasisi ya nje kwa kuzishindanisha blog na website zote nchini Tanzania.

Mashindano hayo yalioendeshwa kwa wasomaji kuzipigia kura blog/website wanazoona zinastahili kushinda kwa vipengele tofauti, yamemalizika huku mtandao huu ukishinda katika tuzo mbili tofauti na kupewa cheti cha ushindi wa nafasi hizo.

Thehabari imeshika nafasi ya pili kwa kuwa blog bora ya ushirikishaji na uhamasishaji jamii katika masuala mbalimbali yanayowagusa, huku ikifanikiwa pia kushika nafasi ya tatu nchini kama Website Bora kwa utoaji wa taarifa kwa jamii.

Uongozi wa dev.kisakuzi.com unapenda kutoa ushindi huu kwa wewe msomaji ambaye ndiye ulieupigia kura nyingi mtandao huu hadi kufanikiwa kushika nafasi hizo mbili, muhimu.

Tuzo nyingine ambayo Thehabari imetwaa.