Thamani ya Uhai Haikadiriki…!

Thamani ya Uhai Haikadiriki
WANASAYANSI wanakadiria kuwa inagharimu zaidi ya dola za marekani trilioni elfu sita kuiga tishu na viungo vya mwili wa binadamu. Gharama hiyo ni mara 77 ya pato la dunia. Pamoja na gharama hii yote, hakuna hakikisho kwamba jambo hili litafanikiwa. Gharama hii haijumuishi akili aliyojaaliwa binadamu. Hii ni kulingana na utafiti uliofanywa na mwanasayansi Harold J. Morowitz wa chuo kikuu cha Yale nchini Marekani.
Nchini Tanzania kuna ongezeko kubwa la kuenea kwa magonjwa yatokanayo na mtindo wa maisha. Magonjwa hayo ni pamoja na kiharusi, ugonjwa wa ubongo, pumu, ini, kisukari, ugonjwa wa moyo, ugonjwa wa kufeli kwa figo, kupooza, msongo wa mawazo, uzito na unene uliopitiliza, shinikizo la damu, saratani, magonjwa sugu ya mapafu (COPD), matatizo ya kusikia, maumivu sugu ya mgongo na mengine mengi.
Kila mwaka, kumekuwa na ongezeko kubwa la vifo linalosababishwa na magonjwa haya ambayo ni rahisi sana kuzuilika. Huu ni wakati muafaka wa kubadilisha hali hii.
Maradhi mengi ya aina hii yanayotokana na jinsi tunavyoendesha maisha yetu ya kila siku. Mlo wetu na maisha kwa ujumla ndio chanzo kikubwa cha magonjwa haya. Watanzania wengi hutumia nyama kwa wingi, mafuta ya mboga, vyakula vya makopo, tumbaku, madawa, pombe na vyakula vyenye sukari.
Wengi wetu tumechagua maisha ambayo yanaongeza uzito na unene uliopitiliza na mwili usiokuwa na mazoezi. Mabadiliko haya yamechangia kwa kiasi kikubwa magonjwa kama saratani ya utumbo, saratani ya tezi dume, saratani ya matiti, saratani ya mapafu na saratani nyinginezo.
Nchini Tanzania Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imeanzisha Mpango Mkakati wa Sekta ya Afya Namba III wa mwezi Julai 2009 hadi Juni 2015 ambao unatoa wito kwa ajili ya mabadiliko ya mitindo mbaya wa maisha kwa kiasi kikubwa ili kupunguza uwezekano wa mtu kupatwa magonjwa yatokanayo na mtindo wa maisha yake. (I)
Kulingana na mpango mkakati huo, watu lazima wawezeshwe ili kubadilisha mfumo wa maisha yao na kuchagua maisha mazuri kwaajili ya afya zao. Sekta ya afya inalenga uwezeshaji kwa watu binafsi, familia na jamii ili kuboresha maisha, kwa njia ya Majadiliano juu ya mabadiliko ya Tabia. Kushirikiana kwa wadau katika mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali ni muhimu katika suala hili ili kuzuia mlipuko wa magonjwa ya kuambukizwa na yasiyo ya kuambukiza.
Wakati tukihadhimisha Siku ya Saratani Duniani, Dk Diwani Msemo, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORIC) alinukuliwa akisema kwamba wagonjwa wengi wa magonjwa ya kansa husababishwa na mtindo wa maisha ya sasa. Belinda Liana, Afisa Mwandamizi wa Mpango (Lishe), Kituo cha Ushauri, Lishe na huduma za afya (CONSENUTH), anatoa wito kwa Watanzania kubadilisha maisha yao kama njia moja ya kupunguza uwezekano wa kupatwa na magonjwa kwa ujumla. Anasema “watu wanapaswa kupunguza matumizi ya vyakula vya mafuta ikiwa ni pamoja na chips, protini hasahasa nyama nyekundu na vitu sukari” (ii)
Kutokana na maisha mabovu ambayo wengi wetu tumeyachagua, Madaktari duniani kote wameguswa na hali hii na kuamua kuonya juu ya maradhi yanayochangiwa na mtindo wa maisha. Hospitali za Apollo ni mmoja wa hospitali zinazohamasisha maisha yenye afya bora.
Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Hospitali za Apollo Dk. Prathap .C. Reddy anasema kuwa, “Uhai ni kitu kisichoweza kununulika na afya njema ni zawadi ya thamani sana kwetu! Afya njema ya mwili na akili inatusaidia kuishi maisha safi, na kufurahi wakati wote. Hivyo basi afya njema ni kitu ambacho tunakihitaji wakati wote”. (iii)
Anaongeza kuwa “Mwenyezi Mungu katujaalia mwili wenye afya nzuri, ambao haujatugharimu hata kidogo. Mwili wetu ni wa thamani sana, lakini kwa bahati mbaya wengi wetu hatuuchukulii hivyo. Tunatakiwa kuthamini mwili wetu, kuulinda na kuuenzi pia. Muhimu zaidi ni lazima kuupatia heshima unayostahili. Tunajua cha kufanya ili tuwe na afya njema lakini hatufanyi. Matokeo yake yanajidhihirisha sasa tumekuwa na afya mbovu iliyosheheni magonjwa. ”
Anamalizia kwa kusema kwamba, “Hata sasa, tunasogeza huduma za afya kwenda ulimwengu wa ‘huduma za afya kwa kila mmoja’ ambayo inahusiana na maumbile tofauti ya watu tofauti. Tunafanya hivi ili kurahisisha uchunguzi bora, matibabu na kinga bora na makini zaidi. Ila hiyo haitoshi. Kwa sisi kuwa na afya bora jambo la muhimu zaidi ni hili; unapaswa kudhibiti afya yako. Unapaswa kuelewa kuwa Afya yako hainunuliki, na kuutendea mwili wako unavyopaswa kutendewa. Tuufanye mwaka huu kuwa wa uponyaji, na siyo tu kutibiwa.

Hii inathibitisha ni kiasi gani tunahitaji kuwa makini kuhusu kuwa na afya njema na kufanya jambo hili liwe kipaumbele chetu. Kama unataka kuepukana na magonjwa ya mtindo wa maisha, ni muhimu kuzingatia mlo kamili kwa afya na mazoezi ya mara kwa mara. Afya njema inaanza kwa Kujizoeza kuupa mwili vitu vyenye umuhimu kwake. Afya bora ni hatua ndogo zinazotusaidia kupiga hatua kubwa kuelekea mbele. Uhai haununuliki. Tujitahidi kuishi kulingana na thamani yake halisi.

Kuhusu Hospitali za Apollo
Hospitali ya Apollo ilifunguliwa mnamo mwaka 1983, na kutoka kipindi hicho imekuwa ikiendeshwa kwa kauli mbiu isemayo “Dhamira yetu ni kuleta huduma ya kisasa karibu kabisa na walengwa. Tunajitolea kutoa huduma bora na mafanikio katika elimu na utafiti kwa ajili ya jamii ya kibinadamu”.

Katika miaka 30 tokea kuanzishwa kwake, hospitali ya Apollo imeandika historia kubwa kupata kuonekana nchini India. Ni moja ya kampuni kubwa ya Afya katika bara la Asia, na pia imeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya afya nchini india.

Katika safari yake, imeweza kuboresha maisha ya watu wapatao milioni 39 kutoka nchi 120.
Inatoa huduma maalum 52 na vitanda vya upasuaji 710
Imefanya upasuaji wa moyo wenye kufikia idadi ya watu 152,000 na panuzi 125, 000 za mishipa myembamba.

Imefanya upasuaji wa wa viungo unaopita kiasi cha idadi ya watu 10,000, upasuaji wa uvimbe wa ubongo, uti wa mgongo na zaidi.

Taasisi ya Apollo ni moja ya taasisi zinazoongoza nchini india, zikiwa na teknolojia za kisasa kama Novalis TX, PET MRI na Upasuaji unaotumia mashine za kiroboti.