TGNP Yaendesha Baraza Kukusanya Maoni ya Wadau Wake

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi. Usu Mallya akizungumza kwenye baraza hilo

baadhi ya washiriki wakiwa wenye baraza

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi. Usu Mallya akizungumza na wajumbe wa baraza hilo.

Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mada anuai

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi. Usu Mallya akizungumza na wanahabari kuhusiana na baraza hilo. Nyumba ni sehemu ya baraza likiendelea

MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) unaendesha baraza kukusanya maoni kutoka kwa wadau wake wa masuala ya jinsia yatakayowasilishwa Tume ya Katiba kwa lengo la kuingizwa kwenye mchakato wa Katiba Mpya.

Akizungumzia baraza hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi. Usu Mallya alisema maoni yanayotolewa katika baraza hilo yanatarajiwa kuwasilishwa Tume ya Katiba Agosti 31, 2013.

Akizungumza Bi. Mallya alisema miongoni mwa masuala wanaoyajadili katika baraza hilo ambayo wataomba yaingizwe katika mchakato wa Katiba Mpya utambuzi wa wanawake katika uzalishaji na kutaka uwepo usawa na kutambuliwa kitaifa.

“…Suala lingine ni utambuzi wa mchango wa wanawake katika uchumi na uelekezaji wa kupunguza mzigo wa kazi, yaani usawa katika bajeti. Wanawake wamekuwa na mchango mkubwa sana kwenye kuzalisha na kuendeleza familia, kuendeleza jamii na hata uzalishaji mali lakini mara nyingi michango hii haitambuliwi…hili tungependa katiba mpya iliangalie,” alisema Mallya.

Alisema baraza hilo litajadili na kuomba uwepo mfumo wa utekelezaji wa masuala ya kijinsia unaotambulika kitaifa, au kuwepo na chombo kama tume chenye nguvu kitakachokuwa kikiitisha na kusimamia masuala ya haki na usawa kwa wanawake na wanaume katika ngazi zote.

Alisema yapo masuala mengi waliyoombwa kwenye mchakato yameingizwa kwenye rasimu iliyopo lakini akasisitiza bado kuna maeneo ya kuangaliwa zaidi tena hasa mchanganuo katika msingi wa haki za kijinsia mgawanyiko wa rasilimali za taifa na kimadaraka.