Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali ya ActionAid Tanzania pamoja ana TGNP Mtandao na Wabia wake wameandaa Kongamano la Ardhi kwa wanawake wa Afrika, lijulikanalo kama wazo la Kilimanjrao yaani Kilimanjro Initiative kwa lengo la kuleta sauti za pamoja za wanawake katika kuleta na kulinda Haki ya Ardhi
Grace Kisetu ambaye ni Meneja wa idara ya Ujenzi wa nguvu ya pamoja kutoka Taasisi ya TGNP Dar es Salaam alisema kuwa wanahitaji kuleta mabadiliko yenye kuchochea Maendeleo ya Wanawake wa Nchi za Afrika ikiwemo Tanzania
“Kongamano hilo linatarajia kufanyika kwa siku nne kuanzia Oktoba 13 hadi 16 mwaka huu ikishirikisha wanawake waliopo pembezoni toka katika kanda tano za Afrika ambazo ni Afrika Kusini, mashariki, kati na kaskazini” alisema Bi Kisetu
Aliongeza kuwa Ardhi ni rasilimali muhimu na kichochezo kikuu katika kuleta maendeleo ya uchumi ambapo Kwa Tanzania asilimia kubwa la pato hutokana na Ardhi huku sekta ya kilimo ikitoa fulsa kubwa ya ajiri
Kwa upande wake Scholastica Haule ambaye ni mratibu wa Haki za wanawake kutoka shirika la ActionAid Tanzania alisema kuwa wamedhamilia kutekeleza kikamilifu kanuni na miongozo ya umoja wa Afrika (AU) juu ya uwekezaji na miongozo ya umiliki wa ardhi , uvuvi na misitu
“tutahakikisha kila kitu kinafanyika kwa wakati na kuwapatia wanajamii taarifa sahihi ya kupata ardhi na vibali vya kumiliki ardhi hasa wale walioathirika na uhusiano wa ardhi hasa tukiangalia haki na usawa kwa watoto, vikundi na walemavu”
Jovita Mlau kutoka SASA foundation yenye makao yake makuu mkoani Arusha alisema kuwa imefika wakati wa kusimamia na kupunguza biashara na mipango ya uuzwaji wa ardhi, kuheshimu haki za umiliki wa ardhi na Matumizi ya Ardhi
“lazima tuimalishe na kuboresha sera na kituo cha rasilimali ya ardhi Afrika ili kutekeleza mikakati ya sera za jinsia na utendaji wa mifumo na miongozo juu ya ardhi barani Afrika pamoja na ukusanyaji wa takwimu zinazozingatia jinsia katika ardhi na umiliki wa rasilimali”
Pia alisema kutungwe na kutekelezwe sheria yenye dhana shiriki ya uwakilishi katika maamuzi ya ardhi na maliasili, utawala kutoka ngazi ya chini hadi ngazi ya kitaifa