TFF Yazinduwa Jenzi Mpya, Saba Wateuliwa CAF

Jezi mpya ya nyumbani.

Jezi mpya ya nyumbani.

Jezi ya mazoezi, nyumbani na ugenini

Jezi ya mazoezi, nyumbani na ugenini

Ndolanga akipokea cheti kutoka kwa mh. said mtanda

Ndolanga akipokea cheti kutoka kwa mh. said mtanda

Rais wa TFF, Jamal Malinzi

Rais wa TFF, Jamal Malinzi

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu nchini TFF leo limezindua jezi mpya za timu za Taifa, zitakazokuwa zikitumika na timu za Taifa katika michuano mbali mbali itakayokua inazikabili.

Uzinduzi huo wa jezi mpya uliofanyika katika ukumbi wa Kilimanjaro jengo la Golden Jubilee uliambatana na uziduzi wa tovuti mpya ya shirikisho, uliongozwa na mgeni rasmi Said Mtanda, mbunge wa jimbo la Mchinga na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya jamii.

Katika uzinduzi huo, kulizunduliwa jezi aina tatu, ambazo ni jezi za ugenini, jezi za nyumbani na jezi zitakazokuwa zikitumika kwa ajili ya mazoezi. Ifuatayo ni hotuba ya Rais wa TFF , Jamal Malinzi aliyoisoma wakati wa uzinduzi wa jezi mpya za timu za Taifa, uzinduzi wa tovuti mpya ya TFF na kutunuku vyeti kwa viongozi mbalimbali, makocha, wachezaji na wadhamini.

WATANZANIA SABA WATEULIWA KAMATI ZA CAF
Shirikisho la mpira barani Afrika CAF limewateua Watanzania saba kuwa wajumbe wa kamati zake mbali mbali kwa kipindi cha miaka miwili 2015-2017. Walioteuliwa pamoja na kamati zao katika mabano ni:

1. Leodeger Tenga- (Makami Mwenyekiti Kamati ya Fedha, Mjumbe wa Kamati ya Uendeshaji Mashindano ya fainali za Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa ndani (CHAN), Mwenyekiti wa Kamati ya Mpira wa Wanawake, na Mjumbe wa Kamati ya Vyama Wanachama).

2. Jamal Malinzi – (Mjumbe kamati ya Uendeshaji Mashindano ya Vijana Umri chini ya miaka 20)

3. Mwesigwa Selestine – (Mjumbe Kamati ya Uendeshaji Mashindano ya Vijana Umri chini ya Miaka 17).

4. Richard Sinamtwa -(Mjumbe Kamati ya Rufaa)

5.Dr Paul Marealle -(Mjumbe Kamati ya Tiba)

6. Lina Kessy -(Mjumbe wa Soka la Wanawake)

7. Crescentius Magori-(Mjumbe Kamati ya Soka la Ufukweni na Soka la Ndani)

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania – TFF linawapongeza wajumbe wote walioteuliwa kuingia katika kamati mbali mbali na linawatakia kila la kheri wanapoiwakilisha nchi yetu.
TFF.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)