TFF YAPELEKA MAFUNZO YA UKOCHA ARUMERU.

soccer-mpira-wa-miguu
Zaidi ya wanamichezo 40 wanategemea kunufaika na mafunzo ya awali ya ukocha wa mpira wa miguu yanayofanyika wilayani Arumeru Mkoani Arusha huku washiriki wa mafunzo hayo wakiwa na matazamio makubwa ya kuendeleza vilabu vya soka hapa nchini.

Mafunzo hayo ya yatafanyika kwa muda wiki mbili yanajumuisha makocha wanafunzi kutoka mikoa ya Tanzania Bara ikiwa ni jitihada za kunusuru sekta ya mchezo wa soka hapa nchini.

Akizungumzia zoezi hilo Mwenyekiti wa Chama Cha Soka Wilaya ya Arumeru, ambaye pia ni mjumbe wa mkutano Mkuu Katika chama cha soka Tanzania (TFF) Peter Temu amesema amefarikija kuwepo na mafunzo katika ngazi ya awali kwa kuwa ndio njia pekee ya kuendeleza mchezo wa soka hapa nchini.

“Ili kuweza kuinua soka nchini lazima tuanzie huku chini tena kwa kuwanoa vijana ambao watakuwa chachu kwa wenzao, ambapo itaongeza kuwahamasisha hata wale waliokuwa wameanza kukata tama juu ya soka letu hapa nchini” Alisema Temu.

Kwa upande wake Leonard Sanjo ambaye ni Kocha Mwanafunzi amesema mafunzo hayo ya yameongeza shauku kwao ya kutoa mchango katika mchezo wa soka hasa ya vijijini,maeneo anakotoka ikiwa ni hatua inayochukuliwa kuweka misingi imara katika kuendeleza mchezo wa mpira.

Mafunzo hayo yalianza mwishoni mwa wiki yakiyoendeshwa na Mkufunzi kutoka TFF George Komba ikiwa ni moja kati ya malengo ya kuendeleza na kuleta maendeleo ya mpira wa miguu hapa nchini.