SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litamfikisha kwenye Kamati ya Maadlili mapema Mwakani baada ya sikukuu ya mwaka Mpya 2016, Mkuu wa Mawasiliano wa klabu ya Yanga, Jerry Muro kutokana na kauli zake za kibaguzi dhidi ya Mkuu wa Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litamfikisha kwenye Kamati ya Maadlili mapema Mwakani baada ya sikukuu ya mwaka Mpya 2016, Mkuu wa Mawasiliano wa klabu ya Yanga, Jerry Muro kutokana na kauli zake za kibaguzi dhidi ya Mkuu wa Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara.
Muro alimshambulia kwa maneno ya kibaguzi Manara wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika mkutano uliofanyika jana makao makuu ya klabu ya Yanga jijini Dar es Salaam. Kauli ya Muro dhidi ya Manara ni kinyume na Katiba ya TFF, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambao zinapiga vita vitendo vya ubaguzi wa aina yoyote katika mpira wa miguu.
Mapema mwaka huu, Muro alifikishwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF kutokana na kumshambulia na kumdhalilisha kupitia vyombo vya habari aliyekuwa Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Fatma Abdallah. Kamati ya Nidhamu ilimwadhibu kwa kumpiga faini ya sh. milioni 5.