SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzabia (TFF), ilimefanya marekebisho kwa mechi za Uwanja wa Taifa ili kutekeleza maagizo ya Serikali kucheza mechi mbili tu za Ligi Kuu ya Vodacom, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. TFF imefanya marekebisho hayo kwa baadhi ya mechi zilizokuwa zichezwe kwenye uwanja huo.
Katika taarifa yake iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo, na kusainiwa na Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura amesema kwa sasa mechi zitakazochezwa Uwanja wa Taifa ni – mechi namba 39- kati ya Azam vs Yanga (Septemba 18), mechi namba 50- Simba vs Mtibwa Sugar (Septemba 25).
Aidha Wambura alizitaja mechi zingine ni pamoja na mechi namba 52- Yanga vs Coastal Union (Septemba 28) na mechi namba 58- Yanga vs Kagera Sugar (Oktoba 13). Nyingine ni mechi namba 62- Simba vs African Lyon (Oktoba 16), mechi namba 65- Yanga vs Toto Africans (Oktoba 20), mechi namba 72- Simba vs JKT Ruvu (Oktoba 22), mechi namba 78- Yanga vs Simba (Oktoba 29) na mechi namba 86- Moro United vs Simba (Novemba 2).
Mechi zifuatazo zitachezwa Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam; mechi namba 35- Simba vs Polisi Dodoma (Septemba 14), mechi namba 29- African Lyon v Yanga (Septemba 15), mechi namba 45- Yanga vs Villa Squad (Septemba 21), mechi namba 66- Simba vs Ruvu Shooting (Oktoba 19) na mechi namba 71- Yanga vs Oljoro JKT (Oktoba 23).
Uongozi wa Azam unaomiliki uwanja wa Chamazi tayari umekubali timu za Simba na Yanga kutumia uwanja huo kwa mechi hizo. Akizungumzia mapato ya mchezo kati ya YANGA na RUVU SHOOTING, ya mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa Septemba 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam amesema imeingiza sh. 23,388,000.
“Watazamaji waliokata tiketi kwa ajili ya kushuhudia mechi hiyo walikuwa 6,566. Viingilio vilikuwa sh. 15,000, sh. 7,000, sh. 5,000 na sh. 3,000.
Boniface Wambura, Ofisa Habari Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),” alisema Wambura.