TFF Kuanza Kupokea Mapingamizi kwa Walioomba Uongozi

Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura

BAADA ya kupitia fomu za waombaji uongozi TFF, Kamati ya Uchaguzi ya TFF leo imetoa orodha ya majina ya walioomba nafasi mbalimbali za uongozi wa Shirikisho hilo ili kutoa nafasi kwa wanaowapinga viongozi kufanya hivyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura leo kwa vyombo vya habari ofisi hiyo imebandika kwenye ubao wa matangazo wa TFF majina ya waombaji ili kutoa fursa kwa kipindi cha pingamizi.

“Mwisho wa kupokea pingamizi dhidi ya waombaji uongozi ni Januari 26, 2013 saa 10 kamili alasiri,” alisema Wambura katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.