Tetemeko laua zaidi ya watu 1,000 Uturuki

Wahanga wa tetemeko Uturuki

TETEMEKO la ardhi lenye ukubwa wa kipimo cha 7.3 cha Richter mashariki mwa Uturuki leo limeua kati ya watu 500 hadi elfu moja.
Profesa, Mustafa Erdik Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Matetemeko ya Ardhi ya Kandilli mjini Istanbul ameuambia mkutano wa waandishi wa habari kwamba watu 500 hadi 1,000 wanakadiriwa kuwa wameuwawa katika tetemeko hilo.

Kwa mujibu wa maafisa tetemeko hilo lenye nguvu kubwa limepiga katika mji wa Van ulioko mashariki mwa Uturuki na kujeruhi watu wengi baada ya majengo kadhaa kuanguka.

Matetemeko makubwa ya ardhi katika mikoa yenye watu wengi na viwanda ya kaskazini magharibi yameuwa watu 20,000 hapo mwaka 1999 nchini Uturuki. Tetemeko jengine kubwa la ardhi katika mji wa Caldiran katika jimbo la Van nchini humo limeuwa watu 3,840 hapo mwaka 1976.
-DW