TCU Yataka Wanaokwenda Kusoma Vyuo vya Nje Kuzingatia Vigezo

Afisa Udahili Mwandamizi wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), Dk. Fabian Mahundu akizungumza katika maonesho ya vyuo Vikuu vya nchini India vilivyofanyika katika Ubalozi wa India Jijini Dar es Salaam.

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link (GEL), Abdulmaalik Mollel akizungumza katika maonesho ya vyuo Vikuu vya nchini India vilivyofanyika katika Ubalozi wa India Jijini Dar es Salaam.

TUME ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU) imesema kuwa wanaokwenda kusoma vyuo vikuu vya nje wanatakiwa kuangaliwa vigezo ambavyo vinahitajika. Hayo yamesemwa na Afisa Udahili Mwandamizi wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini, Dk. Fabian Mahundu wakati wa maonesho ya vyuo vikuu vya nchini India yaliyofanyika katika ubalozi wa nchi hiyo leo jijini Dar es Salaam.

Dk. Mahundu amesema mwanafunzi anayekwenda kusoma vyuo vya nje na ndani anatakiwa kuwa ufaulu wa ā€˜Dā€™ mbili ambazo ni viwango vilivyowekwa. Amesema kuwa mwanafunzi anayekwenda kusoma nje bila kupita katika tume hiyo ilivyowekwa kwa ajili ya kuratibu, akirudi anakuwa anakosa sifa katika mfumo wa elimu nchini.

Kwa upande wa Balozi wa India nchini, Sandeep Arya amesema kuwa Tanzania na India zimekuwa na mahusiano mazuri katika nyanja mbalimbali. Amesema India imekuwa ikitoa elimu bora na kwamba Tanzania ni nchi ambayo inanufaika kwa kupata ufadhili wa watu 25 kila mwaka.

Naye, Mkurugenzi wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel amesema kuwa nchi ya India iangalie uwezekano wa kuongeza idadi ya ufadhili hadi kufikia 100 kutokana na mahitaji yaliyopo.

Amesema kuwa GEL imekuwa katika msisitizo wa mara zote katika kuhakikisha wanafunzi wote wanapita TCU kwa ajili ya kuhakikiwa. Maonesho ya vyuo vikuu vya nchini India yamesimamiwa na kampuni ya Global Education Link (GEL) kwa kuteuliwa na Balozi wa India.