TCRA Yatoa Vyeti kwa Wamiliki na Waendeshaji ‘Blogs’

Picture 042

 

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma (kushoto) akimkabidhi cheti Mhariri Mkuu wa Mtandao wa dev.kisakuzi.com (www.thehabari.com), Joachim Mushi mara baada ya ushiriki wa semina hiyo. Picha ya chini ni muonekano wa cheti kilichotolewa na TCRA.

Picture 044
IMG_0067

 

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma (katikati) pamoja na viongozi anuai wakifuatilia warsha hiyo kwa bloggers. Picha anuai chini ni baadhi ya bloggers wakipokea vyeti vyao.

 

 

 

 

Picture 012

Picture 022

Picture 028

Picture 030

Picture 033

Picture 036

3

 

Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy akifafanua jambo wakati wa Warsha ya wamililiki wa magazeti tando (Bloggers) hapa nchini.

IMG_0006

 

Warsha ikiendelea kwa bloggers

IMG_0022

IMG_0032

Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy akiwa na MD, Liz Wachuka kutoka Tech Walk.
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa vyeti kwa baadhi ya wamiliki na waendeshaji wa mitandao ya jamii (blogs) baada ya kutoa semina ya siku mbili juu ya uelewa na namna ya uendeshaji mitandao hiyo kwa kuzingatia maadili na kimaendeleo.

Semina hiyo ambayo imeandaliwa na TCRA ikiwa ni muendelezo wa kampeni yake ya kupinga matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii nchini imewashirikisha wadau anuai ambao waliwasilisha mada kuwaongezea ujuzi ma-Bloggers katika uendeshaji wa masuala ya mitandao ya jamii kwa manufaa zaidi.

Miongoni mwa wadau waliotoa mada kuwanoa ma-bloggers ni pamoja na Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma Tanzania (SJMC), Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kiongozi Mwakilishi Kutoka Kampuni ya Google Barani Afrika, Kampuni ya Tech Walk, Jamii Forum Tanzania, pamoja na TCRA ambao ni waandaaji wa semina hiyo.

Washiriki (bloggers) wote ukiwemo mtandao wa www.thehabari.com walipewa vyeti vya ushiriki wa semina hiyo.