Tarsis Masela wa Akudo Kuzinduwa Albamu ‘Acha Hizo’

Tarsis Masela

Tarsis Masela

UZINDUZI wa albamu ya Mwanamuziki nyota Tarsis Masela iitwayo ‘Acha Hizo’ unatarajiwa kufanyika kesho kwenye Ukumbi wa Ten Lounge, zamani ukijulikana kama Business Park, uliopo Victoria Jijini Dar es Salaam. Katika uzindu huo bendi ya Mashujaa, Akudo Impack na Jahazi Modern Taarab, zitasindikiza usiku huo maalum wa Tarsis Masela.

Akizungumza Dar es Salaam leo Masela, alisema kuwa maandalizi ya uzinduzi huo amekamilika, huku akiwataka wapenzi wajitokeze kwa wingi kuangalia uzinduzi wake utakavyofana.

Masela ambaye ni Rais wa bendi ya Akudo Impact, anazindua albamu yake hiyo yenye nyimbo saba, ambayo ni ya kwanza kuzindua na kuikamilisha. Alisema kuwa kila mshabiki atakayekuja atapata burudani safi kutoka kwake na hata bendi zinazomsindikiza.

Katika uzinduzi huo viingilio vitakuwa viwili ambavyo ni shilingi 30,000 kwa viti vya
maalum na sh.10,000 kwa kawaida. Katika albamu hiyo kuna nyimbo saba ambazo ni Tabia Mbaya ambayo amemshirikisha

Mzee Yusuf‘Mfalme’ Chaguo Langu, Nimevumilia Lady Jay Dee, nyingine ni Vidole Vitatu, Penzi Langu Limezidi Asali, Mwiko na Tusiachane. Onesho hilo limedhaminiwa na RJ Company, Jambo Leo na Clouds FM.