Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete asubuhi ya Agosti 21, 2012, amepokea kwa mshtuko mkubwa, Masikitiko na Huzuni nyingi Taarifa za Kifo cha Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mheshimiwa Meles Zenawi, kilichotokea jana usiku nje ya Nchi ambako alikuwa anatibiwa.
Kufuatia Taarifa hizo, Mheshimiwa Rais Kikwete, kwa niaba ya wananchi wa Tanzania, Serikali yake na kwa niaba yake mwenyewe amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Ethiopia, Mheshimiwa Girma Wolde-Giorgis.
Katika rambirambi zake kwa Mheshimiwa Wolde-Georgis, Rais Kikwete amesema”Tanzania imepokea kwa Mshtuko mkubwa, Masikitiko na Huzuni nyingi Taarifa za kifo cha Mheshimiwa Meles Zenawi kilichotokea jana usiku.”
“Kwa niaba ya wananchi wa Tanzania, Serikali yangu na mimi mwenyewe, natuma salamu zangu za dhati za rambirambi kwako, kwa Wananchi wa Ethiopia na kupitia kwako kwa Mheshimiwa Azeb Mesfin, mjane wa marehem”amesema Dk.Kikwete