Na Scola Milinga, Wizara ya Fedha
TANZANIA imetoa Ripoti ya Tathimini ya Umasikini kwa upande wa Tanzania bara kwa mwaka 2015, ambayo ni haua muhimu kwa Serikali, wadau wa maendeleo na asasi za kiraia nchini.
Hayo yalisema Waziri wa Fedha Saada Mkuya jana alipokuwa akizindua ripoti hiyo jijini Dar es salaam.
Akitoa shukrani zake kwa niaba ya Serikali kwa Benki ya Dunia, Waziri Saada alisema kuwa kuzinduliwa kwa ripoti hiyo ni ya muhimu kwa Serikali, wadau wa maendeleo na asasi za kiraia ambazo wamekuwa mstari wa mbele katika kuambana na umaskini nchini. Waziri Mkuya alisema kuwa ripoti hiyo inaonesha mambo mengi ikiwemo sera na ufumbuzi wa kiufundi, ambavyo vinapaswa kuwa sehemu ya Serikali katika kutekeleza mikakati mbalimbali katika miaka ijayo.
“Inatia moyo sote kujua kwamba umaskini, kama inavyoelezwa katika maana yake pana nchini, umeanza kupungua kwa jumla,” alisema Waziri Saada.
Kupungua huko kunatokana na wigo mpana wa uchumi kama ilivyojitokeza katika ukuaji katika Pato halisi la Taifa kwa asilimia saba kwa mwaka tangu mwaka 2001. Ukuaji huo ni matokeo ya jitihada za kitaifa iliyojengwa kupitia Mkakati wa Kupunguza Umaskini nchini (MKUKUTA I & II na FYDP I). Kiuhalisia, Watanzania wanaoishi chini ya mstari wa umaskini idadi yao imepungua kutoka 34 asilimia mwaka 2007 hadi asilimia 28.2 mwaka 2011/12.
Ripoti hiyo inaonesha kuwa idadi ya watu maskini bado ni kubwa kutokana na kiwango cha juu hali ya halisi ya maisha ikilinganishwa na kasi ya ongezeko la watu wengi maskini walioko vijijini wenye kipato cha chini.
Ili kuhakikisha mchakato wa ukuaji wa uchumi unakuwa na faida nchini katika ustawi wa jamii katika siku za karibuni, yapo mafanikio katika uboreshaji wa hali ya makazi ya kuishi wananchi ambapo mafanikio hayo yamebainishwa kwa kaya kuboresha nyumba na kuwa na nyumba bora ambazo zimeongezeka kutoka asilimia 34 mwaka 2007 hadi 46 katika 2011/12.
Mafanikio mengine ni watumiaji wa vifaa mbalimbali wameongezeka ikiwemo watumiaji wa simu ya mkononi, majiko ya gesi na umeme, televisheni na redio, majokofu na kompyuta. Tathmini ya Umaskini Tanzania Bara inaonesha na kupungua kama ambapo ukuaji wa uchumi umekuwa ni kichocheo cha kasi hiyo.
Ili kuifanya Tanzania kufikia kuwa nchi uchumi wa kati kama ilivyoelezwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, kama nchi, uvumbuzi wa gesi asilia itasaidia kukuza sekta za viwanda, uchimbaji wa madini ambazo ndiyo kichocheo kikuu cha kufikia malengo hayo nchini.