Tanzania Yasaini Mkataba wa Bilioni 314 Kuzaidia Miradi ya Umeme na Gesi Toka Benki ya Dunia

Waziri wa Fedha, Dk. Wiliam Mgimwa akisaini mojawapo ya mikataba ambapo Serikali ya Tanzania imepata bilioni 341.


SERIKALIya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yapokea shilingi bilioni 314 kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya kusaidia miradi ya Umeme, Gesi, Bajeti ya Serikali pamoja na kuwajengea uwezo wa kuendesha miradi ya gesi. Mkataba huo umesainiwa na Waziri wa Fedha, Dk. Wiliam Mgimwa Waziri wa fedha, pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier Mjini Washington. Yafuatayo ni matukio mbalimbali ya picha yakionesha afya ya usainishaji mradi huo mkubwa kwa Tanzania:

Waziri wa Fedha, Dk. Wiliam Mgimwa akibadilishana nyaraka za mikataba na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier


Waziri wa Fedha, Dk. Wiliam Mgimwa pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier wakitia saini mikataba hiyo.


Kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dk. Silvacius Likwelile, Waziri wa Fedha, Dk. Wiliam Mgimwa, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier pamoja na Msimamizi Mkazi wa Miradi ya Benki ya Dunia Tanzania, Burundi na Uganda Bw. Sajjad Ali Shah wakishuhudia tukia la utiaji saini mikataba hiyo mitatu.


Waziri wa Fedha, Dk. Wiliam Mgimwa akisoma hotuba baada ya kusaini mikataba mitatu ya jumla ya shilingi bilioni 341 huku akishuhudiwa na ujumbe wa Benki ya Dunia ukiongozwa na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier.