Na Anna Nkinda – Maelezo
TANZANIA ni nchi ya kwanza Barani Afrika kuwa na mtambo mpya wa alama za upimaji wa ardhi ambapo jumla ya alama 740 zimewekwa nchi nzima kati ya hizo sita zinapima moja kwa moja kwa kutumia satellite.
Hayo yamesemwa hivi karibuni na Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani kutoka wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk. Selassie Mayunga wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi kuhusiana na maandalizi ya mkutano wa kimataifa wa upimaji ardhi na ramani utakaofanyika mwishoni mwa wiki hii jijini Dar es Salaam.
Dk. Mayunga alisema kuwa Mtu akipima ardhi kwa kutumia alama sita ambazo ni za kisasa anapima kwa urahisi na haraka zaidi na zitarahisisha shughuli ya upimaji wa ardhi nchini pia zitapunguza gharama kwa kiasi kikubwa. Tayari mradi huo umeshakamilika na utazindiliwa Juni 13, 2012.
“Karibu Nchi zote za Afrika hazina alama hivi za upimaji hivi sasa Nchi za Uganda na Ghana zimeanza kuweka alama katika ardhi yao, sisi kama wizara mama inayoshughulika na masuala ya ardhi tutahakikisha kuwa alama hizi zinafanya kazi vizuri.
“Hivi sasa wizara yetu ina mpango wa miaka mitano wa upimaji ardhi nchi nzima. Tutahakikisha kuwa kila kipande cha ardhi kinachomilikiwa na mtu kinapimwa kwa njia ya kisasa na katika kutekeleza hili Serikali imekubali kuanzisha kituo cha kupokea picha kwa njia ya Satelite kitakachojengwa mjini Dodoma katika mwaka huu wa fedha wa 2011/12”, alisema Dk. Mayunga.
Aliendelea kusema kuwa kituo hicho kitasaidia kila kipande cha ardhi kupimwa na kujulikana mahali kilipo pamoja na mmiliki wake. Picha zitakazopingwa kwa kutumia satellite zitaonyesha kila kitu kilichopo juu ya ardhi kama ni uvuvi, elimu, madini na hivyo kurahisisha ukusanyaji wa kodi ambazo zitasaidia kuendeleza sekta mbalimbali za maendeleo ya nchi.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa wameshafanya majaribio ya mradi huo katika wilaya ya Babati mkoani Manyara na Bariadi mkoani Shinyanga ambako mashamba zaidi ya laki moja yamepimwa na wamiliki wamepewa hati za umiliki za kimila ambazo wanaweza kuzitumia kukopa fedha Benki.
Alimalizia kwa kuwataka wananchi kulipia ardhi wanayoimiliki kila mwaka mwezi wa saba unapofika kwani ni lazima kwa kila mtanzania kulipia ada ya viwanja bila kukumbushwa na kutolipa au kuendeleza ardhi uliyopewa na Serikali kutakufanya unyang’anywe na radhi hiyo na atapewa mtu mwingine ambaye atakiendeleza. Serikali imepima jumla ya viwanja laki nane na sabini na mbili elfu na kuvimilikisha kwa wananchi na taasisi mbalimbali tangu kupatikana kwa uhuru wa Tanganyika mwaka 1961.
Nchi za Muungano wa Afrika zinazochangia wanajeshi wa kulinda amani nchini Somalia pamoja na wajumbe wa ukanda wa pembe ya Afrika wamekutana katika mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa kujadili mustakbala wa operesheni hiyo ya kulinda amani.
Pamoja masuale mengine yanaangaziwa ni uhaba wa fedha unaokabili operesheni hiyo. Operesheni hiyo iliyodumu kwa miaka mitano sasa inahitaji wanajeshi zaidi, lakini hadi sasa ni Burundi na Uganda pekee ambazo zinahudumu nchini Somalia.
Lulit Kebede msemaji wa Muungano wa Afrika amesema mkutano huo wa Addis Ababa umewaleta pamoja mawaziri wa ulinzi wa Uganda, Burundi, Kenya Djibouti na Ethiopia kwa lengo la kujadili hali ya kisiasa, operesheni za kijeshi pamoja na mustakbala wa operesheni ya kulinda amani nchini Somalia.
Licha ya mkutano huo kuwa wa faragha, taarifa zinasema wajumbe hao pia walijadili azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo linaidhsinian vikosi hivyo kuendelea kuhudumu nchini Somalia hadi mwezi October mwaka wa 2012.
Mkutano huu unakuja wakati Kenya nayo imetuma majeshi yake nchini Somalia katika harakati za kupambana na kundi la Al-Shabab, baada ya utawala wa Nairobi kulihusisha kundi hilo na visa vua utekaji nyara wa wageni ndani ya ardhi ya Kenya.
Lakini suala lingine nyeti ambalo wajumbe hao wasingeweza kuliepuka kujadili ni ukosefu wa fedha ambao unadaiwa kutatiza operesheni nzima ya kijeshi ya Muungano wa Afrika nchini Somalia.
Maafisa waandamizi wa kijeshi wa operesheni ya AMISOM wamekiri kuwa wana pengo la dola millioni kumi, hali ambayo inakwamisha kupelekwa kwa wanajeshi wa ziada nchini Somalia, pamoja na kuendelea na vita dhidi ya kundi la Al-Shabab katika mji mkuu na maeneo mengine nchini.
Nchi za Djibouti na Sierra Leone ambazo kulingana na mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia balozi Augustine ahiga zilitarajiwa kutuma vikosi vyana Somalia kujiunga na operesheni ya AMSIOM, baado hazijatia taarifa kuhusu lini watajiunga na operesheni hiyo na huenda kuchelewa kwao kumesababishwa na hali hiyo ya ukosefu wa fedha.