Tanzania na China zajivunia mafanikio ya matumizi ya teknolojia katika kilimo

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Eng. Christopher Chiza (kulia) akizungumza jambo na Balozi wa China nchini Tanzania Bw.Lu Youqing wakati wa hafla fupi ya kusherehekea mafanikio ya matumizi ya teknolojia ya kilimo kati ya China na Tanzania kwenye miradi mbalimbali ya kilimo nchini

Viongozi mbalimbali kutoka ubalozi wa China na seraikali ya Tanzania wakiimba wimbo wa Taifa wa Tanzania kabla ya kuanza hafla fupi ya kusherehekea mafanikio ya matumizi ya teknolojia ya kilimo kati ya China na Tanzania kwenye miradi mbalimbali inayofanyika nchini Tanzania.Kutoka kushoto nyuma ni balozi wa China nchini Tanzania Bw.Lu Youqing, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Eng. Christopher Chiza na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. John Haule.

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Eng. Christopher Chiza (kulia) akizungumza na wageni mbalimbali walioalikwa na ubalozi wa China nchini Tanzania kuhusu mikakati ya serikali ya kuboresha kilimo na kuongeza uzalishaji wa mazao wakati wa hafla fupi ya kusherehekea mafanikio ya matumizi ya teknolojia ya kilimo kati ya China na Tanzania katika miradi mbalimbali ya Kilimo inayofanyika Tanzania

Raia kutoka mataifa mbalimbali waliohudhuria hafla fupi ya kusherehekea mafanikio ya matumizi ya teknolojia ya kilimo kutoka nchini China katika miradi mbalimbali inayofanyika nchini Tanzania wakijipatia nakala mbalimbali za machapisho kuhusu shughuli za kilimo, siasa, Utamaduni, Teknolojia na masuala ya kijamii.