Tanzania Mwenyeji Mashindano ya Karate

Rais wa UPAM duniani Prof. Maurizi Mardina akimshikilia shingo Master Hudu Thabit akionesha moja ya mbinu inazotumika kwa kujihami kwa ajili ya usalama.

Rais wa UPAM duniani Prof. Maurizi Mardina akimshikilia shingo Master Hudu Thabit akionesha moja ya mbinu inazotumika kwa kujihami kwa ajili ya usalama.

Rais wa UPAM duniani Prof. Maurizi Mardina (kushoto) baada ya kuonesha mbinu ya kujihami kwa mwandishi wa habari Kibwana Dachi (aliyekaa). Kulia ni Master Hudu Thabit. (Picha zote na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

Na Rose Masaka – MAELEZO

UMOJA wa Wapiganaji wa Sanaa ya Mapigano Duniani (UPAM) unaandaa shindano la kimataifa la wapiganaji ambalo linatarajiwa kufanyika nchini kati ya Mwezi Desemba mwaka huu na mwanzoni mwa mwaka ujao kutokana na ruhusa itakayotolewa na Serikali kwa mamlaka zinazohusika.

Kauli hiyo imetolewa na Rais wa UPAM Prof. Maurizi Mardina alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Profesa Mardina alisema kuwa mchezo wa kupigana ni mchezo mzuri ambao unahitaji kujitoa na uwezo mzuri wa kufikiri na siyo mchezo au mafunzo yanayosababisha uonevu bali ni mafunzo yanayompa mtu uwezo wa kujilinda na kujitetea. Ameongeza kwa kusema kuwa Nchi 102 zinatarajiwa kushiriki mashindano hayo ambapo watashiriki wachezaji 25 wa umri na jinsia zote kutoka katika nchi hizo.

“Walimu wanafundisha vizuri ili kuandaa timu bora na baadhi ya vifaa tayari vimenunulia vyenye thamani ya dola ya kimarekani 25000.” amesema Mardina. Kwa upande wake Katibu Mkuu wa UPAM Tanzania Joe Jolamu ameeleza kuwa mashindano ya ndani tayari yameishaanza na yanaendelea ili kuweza kupata timu moja ya taifa itayocheza katika mashindano ya dunia.

“Wachezaji ambao wataruhusiwa kujiunga na kuingia katika kuchezea timu ya dunia ni wale tu ambao wapo katika kikosi maalumu,” alisema mwalimu.