Tanzania Miongoni mwa Majeshi Bora Duniani

Baadhi ya vikosi vya Jeshi la Wananchi la Tanzania

Baadhi ya vikosi vya Jeshi la Wananchi la Tanzania


MAJESHI Maalum (Special Forces) ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania yanayolinda amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ni miongoni mwa vikosi bora 35 vya majeshi ya nchi mbali duniani vinavyokubali kuwa na ufanisi wa hali ya juu, uwezo mkubwa wa kupigana na vilivyofundishwa vizuri.

Kwa mujibu wa Mtandao wa Imgur Via Distractify, Tanzania na jeshi lake ni nchi pekee ya Afrika kuweza kuwa na majeshi yake miongoni mwa majeshi bora duniani. Chini ya kichwa cha habari “35 Most Badass Elite Fighting Units from Around the World” mwandishi, Micky Wren anaandika kuwa hayo ndiyo majeshi bora duniani, yamefundishwa kwa kiwango cha juu kabisa, yana silaha za kisasa kabisa, yameandaliwa vizuri kwa ajili ya operesheni ngumu za kijeshi na yenye uwezo kukabiliana na adui katika mazingira yoyote kuanzia kumaliza uhuni wa utekaji hadi kuwasambaratisha magaidi wenye uwezo mkubwa. Mwandishi anasema kuwa orodha hiyo haikupangwa kwa mtitiriko wa uwezo wa kijeshi wa kila kikundi.

Vikosi vilivyoko kwenye orodha hiyo ni kile cha Seal cha Jeshi la Maji la Marekani, SAS cha Jeshi la Uingereza, Huntsmen Corps cha Majeshi Maalum ya Denmark, Majeshi Maalum ya Ufaransa, Kikosi cha MARSOC, Majeshi Maalum ya Taiwan ambayo yanatumia kinga za usoni zisizoweza kuingiliwa na risasi na Kikosi cha Irish Army Rangers cha Jamhuri ya Ireland.

Vingine ni Gendarmerie cha Serbia, Kikosi Maalum cha Kukabiliana na Ugaidi cha JTF2 cha Canada, Majeshi Maalum ya Uholanzi, Kikosi cha SBS, Majeshi Maalum ya Jamhuri ya Korea, Majeshi Maalum ya Ufaransa, Majeshi Maalum ya Ubelgiji, Kikosi cha MJK cha Norway, Canadian Joint Response Unit cha Canada, Majeshi Maalum ya Norway, Kikosi cha French Commando Marine, Majeshi Maalum ya New Zealand, Kikosi cha Norwegian Armed Forces Special Command na Kikosi cha Polish Grom cha Poland.

Vingine ni Kikosi cha US Army Special Forces Sniper with Remington Modular Sniper Rifle, Majeshi Maalum ya Marekani, Majeshi Maalum ya Indonesia, Majeshi Maalum ya Romania, Kikosi cha SASR cha Australia, Kikosi cha KSK cha Ujerumani, Majeshi Maalum ya Ujerumani, Majeshi Maalum ya Israel – Shayetet 13, Majeshi Maalum ya Urusi – Spetsnaz, Majeshi Maalum ya Austria – Jagdkommando, Majeshi Maalum ya Iraq, Majeshi Maalum ya Ujerumani ya SEK-M na Majeshi Maalum ya Peru.