TANZANIA ni moja ya nchi tatu za Afrika ambazo zitanufaika na uwekezaji wa mabilioni ya fedha katika sekta ya umeme kutokana na mpango maalum wa kuwekeza kwa kiwango kikubwa katika huduma za umeme katika Afrika kwa nia ya kuongeza kasi ya maendeleo na kupunguza kiwango cha umasikini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameambiwa Jumanne, Septemba 22, 2015, mjini Washington D.C. Marekani kuwa, Tanzania itakuwa miongoni mwa nchi ambazo zitanufaika na uwekezaji ambao utafikia kiasi cha bilioni tano za dola za Marekani.
Mtendaji Mkuu na Mtawala Mkuu wa zamani wa Shirika la Maendeleo ya Misaada ya Kimataifa la Marekani (USAID), Bwana Raj Shah, amemwambia Rais Kikwete kuhusu mpango huo wakati walipokutana katika Hoteli ya Ritz-Carlton, Washington, D.C. Marekani wakati wa ziara fupi ya siku mbili ya Rais Kikwete katika mji mkuu huo wa Marekani akitokea katika jiji la New York.
Bw. Shah ambaye pia ni mjumbe katika Jopo la Watu Mashuhuri Duniani linaloongozwa na Rais Kikwete kuangalia jinsi dunia inavyoweza kukabiliana vizuri zaidi na magonjwa ya milipuko katika siku zijazo amemwambia Rais Kikwete kuwa unaanzishwa mpango mkubwa wa mabilioni ya fedha wa kuzalisha umeme katika Bara la Afrikana India kwa nia ya kuharakisha maendeleo ya maeneo hayo mawili.
“Chini ya mpango maalum unaosimamiwa na Latitude Capital, tunaanzisha juhudi binafsi ambazo uwekezaji wake utafikia dola za Marekani bilioni tano kuzalisha, kusafirisha nakuzambazaumemehasakatika Tanzania, Ghana na Kenya na baadaye nchi nyingine zinazotawaliwa vizuri zaidi katika Afrika,”amesema Bw. Shah na kuongeza:
“Mpango huu unatokana na mpango kabambe wa Power Africa uliotangazwa na Rais Barack Obama wakati wa ziara yake katika Tanzania Julai 1-2, mwaka 2013 na taasisi za Benki ya Dunia, IFC, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ziko tayari kuwekeza mabilioni ya fedha katika kuzalisha umeme katika Afrikana India.”
Bw. Shah amemwambia Rais Kikwete kuwa uamuzi wa kuanzisha mpango huo umetokana na ukweli kuwa waanzilishi wake wamefikia azma kuwa ni vigumu kumaliza umasikini katika Afrika na India bila kupatikana umeme wa kutosha.
“Uzalishaji na utumiaji wa umeme katika Afrika na India ni kidogo sana. Tunataka kuwa katika miaka 15 ijayo, Afrikana India, ziwe na umeme wa kiasi cha sasa cha umeme unaotumika katika Marekani. Tunataka kuwa na mpango wenye kufanya kazi kwa ufanisi sana katika Tanzania.”
Bw. Shah pia amesema kuwa“chini ya mpango huo, uwekezaji utakuwa katika miradi mikubwa ya serikali ya umeme ambayo haina mtaji wa kutosha, kuanzisha miradi mipya na kuanzisha miradi ya pamoja ya Serikali na sekta binafsi.”
Mpango huo unaongozwa na Mtendaji Mkuu Frank Perez ambaye amepata kuwa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya taifa ya kuzalisha umeme ya Abudhabi ya Abudhabi National Power Company ambaye ameandamana na Bw. Shah kuja kumwona Rais Kikwete