Tanzania Kuipigia Debe Misri Kurudishiwa Uanachama AU

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipookea ujumbe toka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Nabil Fahmy alipomtembelea Februari 22, 2013 jioni Ikulu jijini Dar es Salaam. Fahmy amefanya ziara nchini kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili hususan katika nyanja za afya, elimu, uwekezaji na siasa.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Nabil Fahmy na ujumbe wake walipomtembelea Februari 22, 2013 jioni Ikulu jijini Dar es salaam. Fahmy amefanya ziara nchini kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili hususan katika nyanja za afya, elimu, uwekezaji na siasa.

Na Mwandishi Wetu

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ameihakikishia Misri kuwa Tanzania itaunga mkono jitihada za nchi hiyo kurejeshewa uanachama wake katika Umoja wa Afrika (AU) baada ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa kidemokrasia nchini humo Aprili mwaka huu.

Rais Kikwete pia amesisitiza kuwa msimamo wa Tanzania kuhusu matumizi ya maji ya Mto Nile ni kwamba nchi zote ambako Mto huo unapitia, kwa namna moja ama nyingine, zina haki sawa ya kutumia maji ya Mto huo kwa maendeleo ya nchi hizo.

Aidha, Rais Kikwete ameishukuru Misri kwa kuchangia maendeleo ya Tanzania kwa kuunga mkono jitihada hizo kwa misaada katika sekta mbali mbali na hasa sekta za maji na afya. Rais Kikwete ameyasema hayo, Februari 22, 2014, wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Nabil Fahmy ambaye pia amewasilisha ujumbe maalum kwa Rais Kikwete kutoka kwa Rais wa muda wa Misri, Adly Mansour.

Katika mazungumzo hayo, Fahmy aliiomba Tanzania kuunga mkono jitihada za Misri kurejeshewa uanachama wake wa AU kufuatia kusikitishwa kwa uanachama huo baada ya kuondolewa madarakani kwa kiongozi wa nchi hiyo aliyekuwa amechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia, Mheshimiwa Mohamed Morsi mwaka jana.

Rais Kikwete alimhakikishia Waziri Fahmy kuwa Tanzania haitasita kuunga mkono jitihada hizo lakini baada ya Misri kuwa imefanya uchaguzi wa kidemokrasia mwezi Aprili mwaka huu.

“Kwa mujibu wa Makubaliano ya Uanzishwaji wa AU, itakuwa vigumu kwa Misri kurejeshewa uanachama wake katika mazingira ya sasa. Lakini baada ya kuwa kufanyika kwa uchaguzi wa kidemokrasia kuchagua kiongozi mpya, Tanzania itakuwepo kuunga mkono jitihada hizo za Misri,” Rais kikwete alimwambia Waziri Fahmy.

Kuhusu matumizi ya maji ya Mto Nile, Rais Kikwete alisisitiza msimamo wa Tanzania wa kuwa ni haki ya kila nchi ambako Mto huo unapitia kutumia maji yake kwa maendeleo yake. “Tunaamini katika Haki ya Matumizi ya Maji kwa nchi zote ambako Mto huu unapitia. Ni aina ya haki hiyo ambayo inatumika hata Tanzania kulingana na matumizi ya maji ya mito mbali mbali ndani ya Tanzania,”

Mapema Waziri Fahmy alimwambia Rais Kikwete kuhusu umuhimu wa maji ya Mto Nile kwa nchi ya Misri akisema: “Sisi katika Misri hupata mvua kwa siku tatu kwa wastani kwa mwaka. Maji yote tunayotumia yanatokana na Mto Nile. Hivyo, unaweza kuelewa umuhimu wa Mto huo kwa uhaki na ustawi wa nchi yetu.”

Rais Kikwete pia ameishukuru Misri kwa misaada yake ya maendeleo kwa Tanzania hasa katika sekta za afya na maji. Waziri Fahmy yuko katika ziara ya siku tatu katika Tanzania na anatarajiwa kuondoka nchini leo, Jumapili, Februari 23, 2014.