Na James Gashumba, EANA Arusha
SERIKALI ya Tanzania imetangaza mipango mipya itakayorahisisha upakuaji wa mazigo katika bandari ya Dar es Salaam. Waziri wa Uchukuzi wa Tanzania, Dk. Harison Mwakyembe alisema mipango iko mbioni ya kukarabati maeneo ya kupakulia mizigo kutoka moja hadi saba na kujenga maeneo mengine mapya manne ya aina hiyo ili kurahisisha upakuajia wa mizigo.
Alikuwa anazungumza katika Mkutano wa Wakala wa Usafirishaji Mizigo (CCTTFA) uliokuwa unafanyika mjini Kigali, Rwanda mwishoni mwa wiki. Alisema mamlaka ya bandari hiyo pia imetenga eneo lililokaribu na bandari hiyo kwa lengo la kujenga bandari ya nchi kavu ili kuhudumia shehena zinazosafrishwa kwenda katika nchi za Rwanda, Burundi,Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Takwimu zinaonyesha kwamba asilimia 50 ya shehena zinasosafirishwa ndani na nje ya Rwanda zinapitia bandari ya Dar es Salaam kupitia korida la Kati. Dk. Mwakwembe alifafanua kwamba kutokana na juhudi hizo mpya idadi ya siku za kusafirisha shehena kutoka bandari ya Dar es Salaam kwenda Rusumo, mpakani mwa Rwanda na Tanzania zitapungua kutoka siku 3.5 hadi 2.5.
Tunachokihitija, alisema, ni kuhakikisha kwamba korida la kati na bandari zinafanyakazi kwa ufanisi.
“Tunahitaji mwingiliano zaidi, baina ya washikadau wote na serikali zetu,” aliuambia mkutano huo.
Wasafirishaji mizigo awali walilalamika juu ya kuwepo kwa urasimu, rushwa na wizi katika bandari ya Dar es Salaam, mambo ambayo mpango huo mpya unakabiliana nayo kuyadhibiti. Makamu wa Rais wa Chama cha Madereva wa Magari Yaendayosafari Ndefu nchini Rwanda (ACPLRWA), Issa Mugarura alisema wamekuwa wakihakikishiwa huduma hiyo na serikali ya Tanzania wakati wote lakini utekelezaji bado ni changamoto.
Hivi sasa bandari ya Dar es Salaam inapokea shehena ya tani 13.5 milioni kwa mwaka na inatarajiwa kuongezeka na kufikia tani 18 milioni baada ya kukamilika kwa mabadiliko hayo mapya.
Asilimia kubwa ya wakazi wa Wilaya hii hujishughulisha na kilimo. Na hulima mazao ya biashara pamoja na mazao ya chakula. Mazao ya chakula yanayolimwa katika wilaya hii ni pamoja na Mahindi, Mpunga, Maharage, Viazi vitamu na Mhogo. Wakazi pia hulima mazao ya biashara ambayo ni pamoja na Tumbaku, Korosho, Ufuta, Karanga na Nazi. Mazao ya mahindi na mpunga wakati mwingine hutumiwa pia kama mazao ya biashara hasa inapotokea ziada katika uzalishaji.
Hata hivyo asilimia 83.6 ya ardhi ya Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru inafaa kwa kilimo, lakini inayotumika kwa sasa ni asilimia 0.6 tu. Mazao ya biashara ni Kilimo cha umwagiliaji kwa zao la mpunga na Paprika hivi sasa vinapewa kipaumbele hasa baada ya zao la Tumbaku kuwa na utata katika soko. Jumla ya hekta 1200 zinafaa kwa kilimo cha umwagiliaji. Hivi sasa ni hekta 10,100 tu ndiyo zinazotumika kwa kilimo cha umwagiliaji.