Na Mwandishi wetu
MCHEZO wa ngumi nchini Tanzania unazidi kushika kasi kutokana na kuchipuka kwa mabondia wengina mapromota ambao wanapigana katika kuwania mataji mbalimbali nje na ndani ya Tanzania na kuandaa
mapambano.
Wapo mabondia wengi katika historia ya Tanzania ambao wamewahi kupigana nje ya nchi hukiwauliza kuhusu ubora wa mchezo wa ngumi katika upande wa vifaa vya mchezo huo ndani ya nchi yetu ni
imani yangu waliowengi wanaweza kukubaliana nami kuwa bado unahitaji vitu muhimu ili kuendeleza mchezo huo.
Kwa Tanzania tumekuwa na mabondia wengi ambao wameweza kutingisha nje ya Tanzania kama Joseph Marwa, Rashid Matumla, Rogers mtagwa Ally Kimweri na Emanuel Mrundwa ambao waliweza kutwaa mataji mbalimbali ya mchezo huo. Jambo moja kuu ambalo watanzania tunalisahau ni kukosekana kwa kumbi bora ya mchezo huo kwa upande mwingine kuna wakati baadhi ya watu wanaohusika na mchezo wa ngumi waliwahi kuwa na wazo hilo lakini nimeona leo nijaribu kulitilia mkazo.
Natoa mfano kama tulivyo weza kujenga uwanja wa taifa na kuziona nchi kubwa duniani zikija kucheza mechi za kirafiki kama Brazil basi hata mchezo wa ngumi linawezekana ukitazama kama marekani ambao mchezo huu umekuwa kwa kiwango cha juu kutokana nchi hiyo kuboresha maeneo ya kuchezea kumbuka silinganishi kiwango cha mchezo bali ni namna ya kuboresha.
Kwa Tanzania vipo vyama vingi vya mchezo wa ngumi PST, TPBC, TPBO bila kusahau kile cha taifa cha BFT lakini ni mara kadhaa Makore Mashaga katibu mkuu wa BFT amekuwa akizungumzia juu ya ukosefu wa vifaa maeneo ya mazoezi na kumbi za kupigania.
Vitu hivi vimekuwa ni vikwazo vikubwa kwa mchezo huo kwa Tanzania. Lakini kwa kuwa Serikali imeweza kuleta uwanja mpya wa mpira wa miguu ambao hata Suleiman Nyambui anafaidika nao alikadharika wanamuziki kupata studio ya kisasa ya kurekodia muziki bila shaka mchezo wa ngumi nao unahitaji eneo zuri la kuchezea.
Kama ilivyo Las Vegas, Nevada na MGM Grand au Madson Square ni dhahiri inawezakana kumbi kama hizi kuwa Tanzania. Kwa hili kuna haja ya vyama vya mchezo wa ngumi nchini kukaa chini na kujadiliana na Serikali kupitia Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo, kuhakikisha tunapata kumbi bora ya kisasa ya mchezo wa ngumu ili kuongeza ujuzi na viwango vya mchezo wa ngumi nchini.
Kama nchi ya Ufilipino imeweza kutoa Bingwa wa Dunia wa mchezo huu Tanzania pia inaweza kufanya hivyo, kwani ukiacha soka mchezo wa ngumi ndiyo mchezo pekee ambao unakuja kwa kasi kwa sasa.
Hili pengine liwe ombi rasmi kwa Rais wa Tanzania ambaye mwaka jana alitunikiwa tuzo ya heshima ya mwanamichezo na chama cha waandishi wa habari za michezo Tanzania TASWA kuwa kiongozi bora kwa kujari michezo si vibaya, Jakaya Kikwete akatuachia wapenzi wa masumbwi kumbi bora w hata mabondia wanje wajekupambana Tanzania kama zinavyokuja timu kubwa za mpira dunia
kucheza uwanja wa taifa.
nina maliza kwa kusema kuwa ni imani yangu kuwa kwa kujengwa uwanja huo kutawapa mabondia wa tanzania kujiaamini na kuupanua mchezo huo na unaweza pia kulitangaza jina la Tanzania katika Nyanja za utalii ndani na nje ya Tanzania kama inavyowezekana kuleta mastaa wa wakubwa wa muziki kutoka ulaya na amerika ni dhahiri hakuna lisilowekana kwa Tanzania.