Pichani Juu na Chini ni Lundo la matawi ya miti yanayodaiwa kukatwa na Shirika la Umeme Tanesco nakuachwa chini ya kizagaa hovyo bila kujulikana utaratibu wa kuyazoa. Eneo hili ni karibu na Hotel ya Southern Sun kuelekea jengo la Pam Residence maeneo ya Ocean road jijini Dar.
Lundo la matawi ya miti lilotelekezwa na Tanesco katika maeneo ya karibu na ofisi za Shirika la Afya duniani WHO.
Hapa ni ukuta wa Chuo cha usimamizi wa fedha IFM.
Ofisa Habari wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro ltd Vidah Fammie akizungumzia changamoto kampuni hiyo inayokumbana nazo wakati wa kutekelezaji wajibu wao wa kufanya usafi na kutolea mfano kubwa likiwa la matawi ya miti kuachwa hovyo barabarani.
Amesema Kampuni yake inashughulika na Domestic Garbage lakini swala la miti liko nje ya kazi za kampuni hiyo na kuashauri kuwa ingekuwa vizuri mtu anapotaka kukata miti awasiliane nao waweze kushauriana juu ya uzoaji wa taka hizo.
Amesema taka za aina hiyo zinazongeza gharama kwa kampuni ya Green Waste Pro Ltd kwa kuwa magari yake ni maalum kwa ajili ya kubeba Domestic Garbage hivyo yoyote atakayetaka kufanya zoezi la kukata matawi ya miti pembezoni mwa barabara za jiji anapaswa kutoa taarifa mapema.
Kampuni ya Green Waste Pro Ltd imekuwa ikilishitumu shirika la Umeme Tanesco kwa kukata matawi ya miti na kuyaacha yakizagaa katika barabara na kuwa hiyo si mara ya kwanza shirika hilo limekuwa likifanya hivyo mara kadhaa, kwani kipindi cha nyuma waliwahi kuacha matawi barabarani na kampuni hiyo ikawajibika kuingia gharama ya kuzoa taka hizo na ilipowaandikia Invoice ya kwamba wamechafua mji na kampuni hiyo imechukua jukumu la kufanya usafi hivyo inawadai walikaidi kulipa.
Leo kampuni hiyo imeendelea na zoezi la kukata matawi ya miti na kuyaacha katika barabara tofauti za jiji yakizagaa hovyo huku haijulikani nani anawajibika kwenda kuzoa.