TANESCO waanzisha blogu kwa mawasiliano

Haya wajameni, hatimaye TANESCO wamefungua blogu kwa ajili ya mawasiliano ambao anwani yao ni umemeforum.blogspot.com na ujumbe wa utangulizi katika blogu hiyo unasema:

Blogu hii ni kwa ajili ya wadau mbalimbali wa umeme wa ndani na wa nje ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Blogu hii inatoa fursa na uhuru wa wananchi na wateja wetu kutoa maoni yao juu ya huduma za Shirika kwa lengo la kuboresha na si kubomoa. Blogu hii inapokea maoni ya kila aina na changamoto zenye kujenga. Lugha inayoruhusiwa ni ya Taifa (Kiswahili) fasaha au Kiingereza. Lugha ya Matusi si ustaarabu. Uhuru wa kutoa maoni si uhuru wa kutukana. TANESCO – Tunayaangaza Maisha Yako.