MAADHIMISHO ya Kimataifa Siku ya Mtoto wa kike Duniani yalitangazwa na Umoja wa Mataifa mwaka 2011. Maadhimisho ya kwanza ya siku hii yalifanyika Oktoba 2011, TAMWA inaupongeza Umoja wa Mataifa kuanzisha Siku hii muhimu ambayo imelenga kuikumbusha jamii juu ya malezi bora ya mtoto wa kike.
Siku hii ya mtoto wa kike ni siku pekee ya kuikuimbusha jamii kuhusu haki za mtoto wa kike na pia kuwawezesha wasichana kutambua fursa zilipo mbele yao katika ujenzi ya jamii mpya enedelevu yenye kuleta usawa. Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo watoto wa kike wamekuwa wakipitia changamoto mbalimbali zikiwemo kukatishwa masomo, kuozeshwa kwa lazima, ubakaji, ukeketaji pamoja na kutelekezwa na kupelekea kushindwa kutimiza ndoto zake.
Kwa mujibu wa utafiti wa UNICEF uliofanyika 2009 unaonyesha kuwa, wasichana wanne kati ya kumi walifanyiwa ukatili wa kiji sia kabla ya kutimiza miaka 18. Aidha takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 61 ya wanawake wenye umri kati ya miaka 20-24 ambao hawakusoma na asilimia 39 ya wanawake wenye umri kama huo wenye elimu ya msingi tu waliolewa wakiwa na umri chini ya miaka 18 ukilinganisha na wanawake wenye umri kama huo ambao wana elimu ya sekondari au zaidi.
Hali hii inafanya ndoa za utotoni kuwa ni sehemu ya ukatili kwa mtoto wa kike. Aidha katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mtoto kike Duniani, TAMWA inaona kuwa kuna umuhimu wa kuziaangalia upya changamoto kisheria kwani zimekuwa kizingiti kwa mtoto wa kike katika kukuwa kwake, kutambua haki zake za msingi kama vile kupata elimu, malezi bora na mahitaji yote ya msingi, lakini pia kumuwezesha katika kujifunza namna ya kupambana na kila aina ya ukatikili anaokumbana nao ndani ya jamii.
“Kauli mbiu ya mwaka huu katika maadhimisho hayo ni “mimba na ndoa za utotoni zinaepukika, chukua hatua kumlinda mtoto wa kike”