Mgeni rasmi katika hafla ya TAMWA wakizinduwa mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani, Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga akizungumza kabla ya kuzindua mradi huo. TAMWA wamezindua mradi huo ikiwa ni jitihada za kupunguza ajali hizo ambazo zimekuwa zikigharimu maisha ya wanawake, watoto pamoja na jamii nzima.
Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Edda Sanga (kushoto) akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani ikiwa ni jitihada za kupunguza ajali hizo ambazo zimekuwa zikigharimu maisha ya wanawake, watoto pamoja na jamii nzima.
Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Edda Sanga akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani ikiwa ni jitihada za kupunguza ajali hizo ambazo zimekuwa zikigharimu maisha ya wanawake, watoto pamoja na jamii nzima.

Ofisa Miradi Mkuu, TAMWA, Bi. Gradness Munuo (kulia) akitambulisha mradi huo kwa washiriki wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani.
Baadhi ya maofisa kutoka TAMWA (wa kwanza na wa pili kulia) wakifuatilia mijadala anuai pamoja na washiriki wengine katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani.
Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Edda Sanga (kushoto) akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani ikiwa ni jitihada za kupunguza ajali hizo ambazo zimekuwa zikigharimu maisha ya wanawake, watoto pamoja na jamii nzima.
Baadhi ya washiriki wa hafla ya TAMWA wakizinduwa mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wadau anuai.

CHAMA cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimezindua mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani ikiwa ni jitihada za kupunguza ajali za vyombo hivyo ambazo zimekuwa zikigharimu maisha ya wanawake, watoto pamoja na jamii nzima. Akizindua mradi huo Makao Makuu ya Ofisi za TAMWA, Sinza jijini Dar es Salaam Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga amepongeza jitihada hizo kwani zitasaidia kuongeza elimu juu ya masuala ya usalama barabarani na namna ya kukabiliana na ajali.
Akizungumza awali Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Edda Sanga alisema chama hicho kimeguswa kushiriki katika mapambano ya ajali za barabarani kutokana na kuona ipo idadi ya wanawake wengi na watoto wamekuwa wakiathiriwa na ajali hizo kila uchao. Alisema ujio wa usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda watumiaji wengi wa usafiri huo ni wanawake wanapokuwa katika shughuli zao za kila siku na ndio wanaoguswa na ajali hizo.
Alisema wapo wakina mama ambao wamekuwa wakifanya biashara zao pembezoni wa barabara kundi ambalo nalo limekuwa likiathiriwa kwa kiasi kikubwa na ajali za barabarani zinapotokea. Akifafanua zaidi alisema chama hicho kitajikita katika kutoa elimu ya usalama barabarani; ikiwa ni pamoja kupinga ulevi wakati wa uendeshaji vyombo vya moto, kuhamasisha uvaaji wa kofia ngumu (helment) kwa waendesha pikipiki pamoja na abiria wao, kuhamasisha ufungaji mikanda kwenye magari pamoja na kuelimisha jamii kuwa mwendo wa kasi barabarani ni hatari.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika tukio hilo, Kamanda Mohammed Mpinga alisema kuna kila sababu ya wadau kama TAMWA kujitokeza kupambana na ajali za barabarani kwani zinamguza kila mmoja. Alisema licha ya idadi ya ajali kuendelea kupungua mwaka hadi mwaka ukilinganisha, lakini bado kuna roho na mali za raia zinapotea kila wakati hivyo kuna kila sababu ya elimu ya usalama barabarani na mapambano yakafanywa kwa ushirikiano wa wadau wote.
Alitolea mfano kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Januari 2016, jumla ya ajali za barabarani zilizotokea ni 5,152, ambapo vifo vilikuwa 1,580 na majeruhi ni 4,659 huku vifo hivyo vikigharimu maisha ya wanawake 301. Uzinduzi huo ambao uliambatana na kutoa mada mbalimbali juu ya mikakati na mapambani katika mradi huo, wakiwemo viongozi wa Serikali, madereva na mashirika anuai yasiyo ya kiserikali pamoja na waandishi wa habari.