TAMISEMI Yawataka Wananchi Kufanya Usafi Endelevu

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Bw. Zuberi Samataba(kulia) akitoa agizo kwa Mkuu wa Idara ya Usafishaji na Manispaa ya Manispaa ya Temeke Bw. Ally Hatibu ya kuondoa mara moja uchafu katika eneo la barabara ya Kiburugwa ambayo wakazi wa huko wamegeuza sehemu ya kutupa takataka. Agizo hilo alilitoa jana wakati alipofanya ziara ya kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la usafishaji wa mazingira. Picha zote na Beatrice Lyimo -MAELEZO

Katapila la Halmashauri la Manispaa ya Temeke likizoa uchafu jana katika soko la Temeke Sterio ikiwa ni utekelezaji agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli la usafishaji wa mazingira.

Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, Dar es salaam

SERIKALI imewataka wananchi wote kuwajibika katika usafishaji wa mazingira na maeneo yanayowazunguka ili kudhibiti magonjwa mbalimbali ya mlipuko ikiwemo kipindupindu. Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Zuberi Samataba wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ya ukaguzi na utoaji mwongozo katika kutekeleza agizo la Rais la kutumia siku ya Uhuru kufanya usafi.

Alisema kuwa kila mwanachi anapaswa kuhakikisha mazingira anayoishi na yale yanayomzunguka yanakuwa safi wakati wote ili kupunguza mlipuko wa kipindupindu. Samataba alisema kuwa mazingira yanayowazunguka wananchi yakiwa safi yatapunguza matumizi ya serikali yanatokana na ununuzi wa dawa za kutibu wagonjwa wa kipindupindu na hivyo fedha hizo kuelekezwa katika matumizi mengine.

“Kila mmoja akiwajibika mahali pa kazi na mazingira yanayomzunguka hali hii itasaidia kuimarishwa usafi na hivyo kila mtu anapaswa awajibike kwa uchafu anaouzalisha nyumbani kwake au sehemu ya kazi yake kwani jukumu la usafi ni la kila mtu,” alisisitiza Samataba.

Alisema kuwa kila Halmashauri nchini inapaswa kujipanga vizuri katika kuhakikisha kuwa inaondoa uchafu mitaani na kusafisha maeneo yake ili kuondokana na tatizo la kipindupindu. Samataba aliwaagiza viongozi wa Manispaa ya Temeke na Halmashauri nyingine nchini kusimamia suala la usafi kuhakikisha linakuwa endelevu kwani jukumu la usimamizi wa usafi ni la kila mtu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Photidas Kagimbo alisema kuwa wananchi wa Halamashauri hiyo wamelipokea suala la utekelezaji wa agizo la Rais na wanaahidi kuhakikisha kuwa maeneo yote yanakuwa safi siku zote.