Na Atley Kuni, Ofisa Habari Mwanza
HALMASHAURI za majiji na manispaa zimehimizwa kutunza na kuhifadhi miradi yote ya maendeleo inayo tekelezwa katika maeneo yao na kuhakikisha inadumu kwa manufaa ya kizazi cha leo na kijacho.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Zuberi Samataba katika hoteli ya Gold Crest Jijini Mwanza wakati wa kikao cha pamoja baina ya TAMISEMI, Benki ya Dunia (World Bank) DANIDA na watendaji kutoka halmashauri zinazo tekeleza miradi ya Tanzania Strategic Cities Project (TSCP).
Samataba, amesema, kuna haja kwa kila halmashauri kuhakikisha inatunza miradi yote ambayo inafadhiliwa na wahisani hata baada ya wahisani kumaliza muda wao na kuondoka kasha miradi hiyo mikononi mwa Halmashauri. “Nivema mkawa mnatenga fedha kwa ajili yakuhudumia miradi inayo anzishwa na wafadhili kwa ajili ya ukarabati na kuimarisha ili iendelee kudumu kwa muda mrefu hata baada ya miradi hiyo kuisha muda wake na wafadhili kuicha mikononi mwetu”.
Katika hatua nyingine amewaagiza watendaji hao kutoa taarifa kwa wakati ili kujenga imani kwa wafadhili wanao toa fedha zao kwa ajili ya miradi mbali mbali ya maendeleo wanayo ifadhili, “Wenzetu suala la mrejesho ni muhimu sana lakini zaidi sana mrejesho kwa wakati, kwani ni kama wanasheria wanavyo amini kuwa HAKI ILIYO CHELEWESHWA NI HAKI ILIYO NYIMWA”.
Kwa mantiki hiyo kutoa taarifa kwa wakati ni suala muhimu sana, vinginevyo au kinyume chake nikuwafanya wafadhili kupoteza imani kwa wanao wafadhili kwenye miradi amesema na kuongeza kuwa kwakuwa serikaliinaondoka kwenye utendaji wa kawaida na kuelekea kwenye utendaji wa upimaji ufanisi kwa matokeo (Performance for Result) hivyo moja ya kigezo muhimu kitakachotumika ni kupima matokeo ni uwasilishaji wa taarifa kwa wakati.
Kikao hicho cha siku tatu kina wakutanisha Watendaji kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Halmashauri Jiji la Mwanza, Manispaa ya Ilemela, Manispaaya Kigoma Ujiji, Manispaa ya Dodoma, (CDA), Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Halmashauri ya mikindani Mtwara, Jiji la Tanga, Jiji la Arusha pamoja na wawakilishi wa DANIDA sambamba na World Bank.