TAMASHA kubwa la vipaji linatarajia kufanyika katika Ukumbi wa Ikondolelo Lodge Hoteli ya Kitalii Kibamba Jumapili hii. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano, Fredy Tony Njeje, waandaaji wa Tamasha la Miss Utalii nchini.
Alisema warembo zaidi ya 30 wanatarajia kuingia katika kinyang’anyiro kuonesha vipaji anuai ikiwemo kucheza ngoma, Kuimba, pamoja kuonesha mavazi mbalimbali ya Asilia.
Alisema kuwa katika Tamasha hilo Maalum Mgeni Rasmi atakuwa ni Mbunge wa Jimbo la kinondoni, Iddy Azan Zungu. Aidha aliongeza kuwa sambamba na hayo Zungu atazindua tuzo mbalimbali za Utalii Tanzania, kama Tuzo ya Mazingira, Tuzo ya Utamaduni, Tuzo ya Jinsia, wanawake na watoto, Tuzo ya Polisi Jamii, Tuzo ya Elimu ya Jamii, Tuzo ya Hifadhi ya Serengeti, Tuzo ya Mlima Kilimanjaro, Tuzo ya Michezo pamoja na Tuzo zengine mbalimbali.
Viingilio katika Tamasha hilo vitakuwa kama ifuatavyo, V.I.P 20,000, Watu wa kawaida 10,000 na watoto 5,000, Tamasha litaanza kuanzia sa nane mchana na kuendelea.