Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ni Funika Dodoma!

Baadhi ya mashabiki wakishangweka vilivyo usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta usiku huu ndani ya Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

 

Wasanii mahiri wa filamu hapa nchini nao walikuwepo kuliunga mkono tamasha la Fiesta usiku huu ndani ya Dodoma, kutoka kulia ni Jacob Steven a. k. a JB, Wema Sepetu pamoja Aunt Ezekiel.
Ray Kigosi akilicheza sebene jukwaani.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi akisoma jina la mshindi wa gari aina ya Vitz inayotolewa na kampuni ya Push Mobile, ikiwa ni sehemu ya mchakato wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012, pichani kati ni Meneja masoko wa kampuni ya Push Mobile, Rodney Lugambo, mwakilishi wa Michezo ya Bahati Nasibu ya Taifa, Humudi pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Lephy Gembe.
 Pichani juu na chini Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Linah kutoka THT akitumbuiza jukwaani usiku huu wakati wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012 likiendelea usiku

 

 Pichani juu na chini ni msanii anaetamba katika miondoko ya R&B hapa bongo, aitwaye Ben Paul akiwarusha wakazi wa mji wa Dodoma waliojitokeza kwa wingi kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta linaleondelea usiku huu kwenye uwanja wa Jamuhuri.
Msanii Shetta akiwaimbisha washabiki wake usiku huu.
Rich Mavoco akiwaimbisha washabiki wake kibao waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 linalofanyika usiku huu ndani ya uwanja wa Jamhuri.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Dayna akijitokeza kwa mbwembwe jukwaani usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 linaloendelea hivi sasa kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, ambapo wakazi wake wamejitokeza kwa wingi kuwashuhudia wasanii mbalimbali wanaotumbuiza kwenye jukwaa hilo.
 Wakazi wa mji wa Dodoma wakiwa wamejitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Huyu ni Recho kutoka nyumba ya Vipati THT, akiimba jukwaani kwa madaha, huku umati (haupo pichani)ukishangilia kwa nguvu.

 Msanii wa muziki wa kizazi kipya akiwa amebebwa juu  mara baada ya kujitokeza jukwaani na wasanii waliopa  mtafu kutoka THT.