Watanzania waishio mjini Kairo, Misri jana walijumuika na wenzao wa mataifa mengine kutoka Afrika katika mchezo wa mpira wa miguu, ambao kabumbu huwa linapigwa mpaka mshindi apatikane (Tournament). Katika tamasha hilo nchi za Rwanda, Burundi, Zimbabwe, Tanzania, na nyinginezo zilishiriki. Kwa bahati mbaya, Tanzania ilitolewa katika kinyang’anyiro hicho, na timu ya Burundi ilifanikiwa kunyakuwa kombe hilo baada ya kuonyesha umahiri mkubwa katika kulisakata kabumbu. Hii ilikuwa katika kufunga sherehe za Iddi El Hajj iliyosheherekewa Misri tokea Jumamosi.
Picha Zote na Habari: dev.kisakuzi.com, Misri