UONGOZI na waandaaji wa Tamasha la Kimataifa la Filamu za Nchi za Jahazi (ZIFF) umewaomba wadau wa tasnia ya filamu na sanaa nchini kushiriki katika Tamasha la 20 la mwaka huu kwani limekuja kivingine na kunafursa nyingi ambazo wanaweza kuzitumia katika kukuza tasmia hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa ZIFF Daniel Nyalusi ameeleza kuwa kwa mwaka huu katika kusherekea miaka ya 20 ya ZIFF kutakuwa na SOKO FILAMU ambayo ni fursa ya adhimu kwa masuala ya filamu na maudhui ya luninga.
Fursa nyingine kwa mwaka huu ni ‘FILM SCHOOLS’ ambapo wanafunzi wa vyuo vya filamu watakutanishwa na fursa ya moja kwa moja ya kuingia katika tasnia hiyo kwa kuwafundisha na kuwakutanisha na watu.
Pia Nyalusi ameongeza kuwa wadau wa tasnia wamekuwa wanatengeneza filamu na kutojua pakuziuzia filamu hizo ila kwa mwaka huu ZIFF imekuja na muarobaini wa changamoto hiyo kwa kushirikiana na DISCOP ambao wanajihusisha na masuala ya uuzaji wa filamu hivyo kile kilio cha kutokuwepo kwa soko la filamu kitakwisha ifikapo mwakani ambapo DISCOP wataingia rasmi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa ZIFF Fabrizio Colombo amesema kwa mwaka huu kutakuwa na tuzo nyingi ambazo zitahusisha upewaji wa kiwango cha fedha huku kiwango cha fedha kuanzia dola 3000 kutolewa, na tuzo za wanawake mshindi kupewa dola 2000 na nyingine nyingi tofauti na awali ambapo haikuwa hivyo.
Tamasha la ZIFF mwaka huu 2017, ni la 20, tokea kuanzishwa kwake na ufanyika kila mwaka katika viunga vya Ngome Kon