Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) Sudi Madega (katikati) akitoa tamko leo jijini Dar es Salaam la kusitishwa kwa maandamano ya amani kuelekea Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa yaliyotakiwa kufanyika Machi 3, 2012. Wengine katika picha ni Ofisa Habari na Uhusiano wa Kitaifa (TALGWU), Shani Kibwasali (kulia) na Ofisa Habari Mkuu wa MAELEZO Mwirabi Sise. Chama hicho kimesitisha maandamano baada ya kufikia muafaka na Serikali. Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es Salaam.