Takwimu Waanza Kusambaza Matokeo ya Sensa Mpya ya 2012

Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 Hajjat Amina Mrisho Said akitoa maelezo mafupi kuhusu Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 iliyofanyika leo katika ukumbi wa Hazina ndogo Dodoma.

Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa akiwahutubia washiriki wa Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 iliyofanyika leo katika ukumbi wa Hazina ndogo Dodoma.

Baadhi ya washiriki wa Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 wakifuatilia kwa makini semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Hazina ndogo Dodoma. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO)

Na VERONICA KAZIMOTO, Dodoma

OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS) mkoani Dodoma imeendesha semina ya usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi 2012 kwa viongozi na watendaji wa ngazi mbalimbali wa mkoa huo kwa lengo la kuwajengea uelewa viongozi hao waweze kuyatumia matokeo ya Sensa hiyo kupanga mipango ya maendeleo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa Semina hiyo viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akiwemo Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Bw.Ephraim Kwesigabo na Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi 2012 Hajjat Amina Mrisho Said wamesema viongozi na watendaji hao wanayo kubwa ya kusimamia matumizi ya takwimu sahihi za Sensa hiyo.

Wamewasisitiza viongozi na watendaji hao kuzitumia takwimu za Sensa ya Watu na Makazi 2012 katika kupanga mipango yao ya maendeleo ili waweze kutatua changamoto balimbali zinazowakabili wananchi wa maeneo wanayoyasimamia.

Aidha, wametoa wito kwa viongozi hao kuzingatia matumizi ya takwimu sahihi pindi wanapotenga fedha za bajeti kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya afya, maji, elimu, kilimo,mifugo na biashara ili bajeti zao ziweze kukidhi mahitaji halisi ya idadi ya wananchi wanaowahudumia. Zoezi la Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi 2012 mbali na mkoa wa Dodoma limeshafanyika katika mkoa wa Pwani na Morogoro.