MECHI ya kirafiki ya kimataifa kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Malawi (The Flames) iliyochezwa Mei 26 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 40,980,000.
Mapato hayo yametokana na washabiki 10,767 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa viingilio vya sh. 3,000, sh. 5,000, sh. 51,000 na sh. 20,000. Washabiki 9,365 walikata tiketi za sh. 3,000.
Asilimia 18 ya mapato hayo ambayo ni sh. 6,251,186 ilikwenda kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) wakati gharama kabla ya mgawo zilikuwa tiketi (sh. 4,999,800), waamuzi (sh. 1,105,000), usafi na ulinzi (sh. 2,350,000), maandalizi ya uwanja- pitch preparation (sh. 400,000), Wachina- Beijing Construction (sh. 2,000,000) na umeme (sh. 300,000).
Kwa upande wa mgawo asilimia 20 ya gharama za mechi ni sh. 4,714,803, asilimia 10 ya uwanja sh. 2,357,401, asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 1,178,701, asilimia 20 ya Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 4,714,803 na asilimia 45 ya TFF (sh. 10,608,306).
TWIGA STARS UWANJANI ETHIOPIA LEO
Twiga Stars inacheza leo (Mei 27 mwaka huu) na Ethiopia katika mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) kuwania tiketi ya kucheza fainali zitakazofanyika Novemba mwaka huu nchini Equatorial Guinea.
Mechi hiyo itakayoanza saa 10 jioni kwa saa za nyumbani itafanyika kwenye Uwanja wa Taifa ulioko jijini Addis Ababa na timu hizo zitarudiana Juni 16 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Addis Ababa, wachezaji wa Twiga Stars ambayo imefikia hoteli ya Churchil, leo saa 4 asubuhi wamefanya mkutano wa mwisho wa maandalizi ya mechi hiyo na kocha wao Charles Boniface Mkwasa na baadaye kupata chakula cha mchana kwa Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia.
Twiga Stars; Fatuma Omari, Mwajuma Abdallah, Fatuma Bashiri, Fatuma Khatib, Evelyn Sekikubo, Mwapewa Mtumwa, Etoe Mlenzi, Mwanahamisi Omari, Ester Chabruma, Fatuma Mustafa na Asha Rashid.
Wachezaji wa akiba ni Maimuna Said, Semeni Abeid, Zena Khamis, Amina Ally, Rukia Hamis na Fadhila Hamad.
Mchezo huo unachezeshwa na Angelique Tuyishime akisaidiwa na Sandrine Murangwa, Speciose Nyinawabari na Salma Mukansanga wote kutoka Rwanda. Kamishna ni Catherine Adipo kutoka Uganda.
Nawakati huo huo Ligi ya Taifa inayoshirikisha mabingwa wa mikoa inaanza kutimua vumbi leo kwenye vituo vya Kigoma, Musoma na Mtwara.
Katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma, Flamingo ya Arusha inacheza na Forest ya Kilimanjaro (saa 8 mchana) wakati saa 10 jioni ni Ashanti United ya Ilala na Polisi ya Mara.
Kituo cha Kigoma leo kina mechi moja tu kati ya Mwadui ya Shinyanga na JKT Kanembwa ya Kigoma itakayochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika kuanzia saa 10 kamili jioni.
Tenende ya Mbeya na Kurugenzi ya Iringa ndizo zitakazoanza saa 8 mchana kwenye Kituo cha Mtwara na kufuatia na mechi kati ya Mpanda Stars ya Rukwa na Ndani ya Mtwara kuanzia saa 10 kamili jioni. Mechi hizo zinachezwa katika Uwanja wa Umoja