Taifa Stars Kushuka Dimbani Dhidi ya Super Eagles

starz

Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, kesho Septemba 3, 2016 inatarajiwa kuingia kibaruani kwa kucheza na Super Eagles ya Nigeria katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017).

Mchezo huo utafanyika kuanzia saa 11.00 (17h00) jioni kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Godswill Akpabo, mjini Uyo katika Jimbo la Akwa Ibom. Muda huo uko mbele kwa saa mbili kamili kwa maana hiyo Taifa Stars itacheza dhidi ya Nigeria saa 9.00 alasiri (15h00).

Taifa Stars iliyoondoka Dar es Salaam, Tanzania jana alfajiri, na wachezaji 18 kabla ya kuungana na Nahodha wa timu hiyo, Mbwana Samatta nchini Nigeria, ilitua salama mjini Uyo ambako imefikia Hoteli ya Le Meridien Ibom & Golf Resort. Samatta – Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayechezea timu ya Genk ya Ubelgiji ya jijini Brussels.

Licha ya mchezo huo kuwa sehemu ya mchuano wa kuwania nafasi ya kucheza fainali hizo za AFCON 2017 huko Gabon, lakini utakuwa ni wa kukamilisha ratiba baada ya Misri kufuzu kwa fainali hizo kutoka kundi G ambalo mbali ya Nigeria na Tanzania, pia ilikuwako Chad ambayo iliyojitoa katikati ya mashindano.
Wachezaji waliosafiri ni:

Makipa-
Said Kipao – JKT Ruvu
Aishi Manula – Azam FC

Mabeki
Vicent Andrew – Young Africans
Mwinyi Haji – Young Africans
Mohamed Hussein – Simba SC
Shomari Kapombe – Azam FC
David Mwantika – Azam FC

Viungo
Himid Mao – Azam FC
Shiza Kichuya – Simba SC
Ibrahim Jeba – Mtibwa Sugar
Jonas Mkude – Simba SC
Muzamiru Yassin – Simba SC
Juma Mahadhi – Young Africans
Farid Mussa Tenerif ya Hispania

Washambuliaji
Jamal Mnyate – Simba
Simon Msuva – Young Africans
Ibrahim Ajib – Simba SC
John Bocco – Azam FC
Mbwana Samatta –KRC Genk ya Ubelgiji

Viongozi walioko na timu hiyo ni:

Ahmed Mgoyi – Mkuu wa msafara
Charles Boniface Mkwasa- Kocha Mkuu
Hemedi Morocco – Kocha Msaidizi
Hussein Swedi – Mtunza Vifaa
Richard Yomba – Daktari wa timu