Zitto Kabwe Asema Serikali ya JPM Inamawaziri Hewa…!

KIONGOZI wa Chama cha ACT Wazalendo, Kabwe Zuberi Zitto (Mb) amesema mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli hawana mamlaka ya uwaziri kuweza kufanya kazi kwa kile kutokuwa na ‘Instruments’ jambo ambalo linawafanya kuwa mawaziri hewa. Zitto ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akiwahutubia wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya …

Zitto Ataja Sababu za Kujiunga ACT…!

ALIYAUWA Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ametaja sababu tano za kujiunga na chama cha ACT-Tanzania huku akijigamba kuwa yeye ni mchapakazi na kwamba sasa mambo yote ni mbele kwa mbele. Akimnukuu Rais wa zamani wa Ghana, Hayati Kwame Nkrumah aliyewahi kusema, ‘forward forever, backward never’, jana Zitto alisema, sasa ni wakati wa kuangalia mbele, hakuna kurudi nyuma tena huku …

Hiki Ndicho Zitto Kabwe Alichowaambia Wapiga Kura Wake Kigoma…!

HOTUBA YA MH ZITTO KABWE (MBUNGE KIGOMA KASKAZINI) ILIYOTOLEWA LEO TAREHE 15 MACHI 2015 MWANAMAPINDUZI na Rais wa zamani wa Burkina Faso Thomas Sankara alisema kuwa ili kuleta mabadiliko ya kimapinduzi ni lazima kuwa na hali fulani ya uendawazimu. Ila tusiufikirie uendawazimu huu wa kuokota makopo bali ule ukichaa mzuri wa kuamini katika mambo au misingi fulani na kuisimamia kwa dhati pamoja …

Zitto Kabwe Njiapanda, Chadema Wamfukuza

HALI ya kisiasa ya mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe imewekwa njiapanda baada ya Chadema kutangaza kumvua uanachama saa chache baada ya Mahakama Kuu kutupilia mbali kesi aliyofungua dhidi ya chama hicho kikuu cha upinzani. Zitto, ambaye amedumu kwenye nafasi ya ubunge kwa takriban mwaka mmoja kutokana na amri ya mahakama, sasa atalazimika kuamua kutangaza rasmi kujiunga na chama kipya …

Tunaweza Kujitosheleza kwa Sukari – Zitto Kabwe

LEO siku nzima kamati ya PAC ilikuwa inazungumza na Bodi ya Sukari, Wizara ya Kilimo na Wakulima wa Miwa Wilayani Kilombero. Tanzania huzalisha wastani wa tani 300,000 za Sukari kwa mwaka ilhali mahitaji ni tani 420,000 kwa mwaka. Hii hupelekea uagizaji wa Sukari kutoka nje ambao umekumbwa na malalamiko makubwa sana kutoka kwa wadau mbalimbali. Masuala kadhaa yameibuliwa katika kikao …