MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (CHADEMA), amewaomba wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba watakaporejea Agosti 5, wapitishe rasimu ya pili ya katiba kama njia ya kumuenzi mama yake Shida Salum, aliyefariki juzi jijini Dar es Salaam. Shida, aliteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, kuwa mjumbe wa Bunge hilo kutoka kundi la wajumbe 201 ambapo aliwawakilisha walemavu, japo alishindwa kuhudhuria kikamilifu …