Sera Mbaya Ndizo Zinazoulea, Kukuza Ugaidi – Kikwete

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete amesema moja ya vyanzo vikubwa vya kuzalisha, kulea na kukuza ugaidi duniani ni sera mbaya za ubaguzi na zinazowanyima haki za msingi baadhi ya wanajamii ama makundi ya wanajamii. Aidha, Rais Kikwete alisema kuwa ni muhimu kwa mataifa mbali mbali duniani kubuni na kutunga sera ambazo zinalenga kutoa nafasi na haki …