Majambazi Yateka Kituo cha Polisi, Yaua Askari na Kuiba Bunduki

HILI linawezekana kuwa ni tukio la kwanza na la aina yake. Majambazi wanaokisiwa kuwa sita, wakiwa na pikipiki tatu, juzi walivamia Kituo Kidogo cha Polisi Mkamba kilichopo Kimanzichana, Wilaya ya Mkuranga, Pwani na kuua askari mmoja na mgambo na kujeruhi mgambo mwingine na kisha kupora bunduki tano na risasi 60 usiku wa kuamkia juzi. Polisi aliyeuawa ni Konstebo Joseph Ngonyani …