Waziri Pinda Ataka Watanzania Kuandika Wosia Kabla ya Kifo

Na Mwandishi Maalum WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda amewataka Watanzania wote nchini wajenge tabia ya kuandika wosia ili kuondoa matatizo ya mirathi pindi mume anapoaga dunia. Ametoa wito huo Mei 29, 2015 wakati akizindua kampeni ya kuandika wosia kwenye maadhimisho ya miaka 25 ya Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) yaliyofanyika katika viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam. …