Waziri Ummy Mwalimu Akipokea Nyumba 20 Kijiji cha Sese, Magu

    Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati), akikata utepe kuashiria upokeaji wa nyumba 20 mkoani Mwanza, zilizojengwa na Taasisi ya Benjamini Mkapa. Nyumba 10 zimejengwa katika wilaya ya Ukerewe na 10 katika wilaya ya Magu. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati), akikata utepe kuashiria upokeaji …

Mradi Kuongeza Ujuzi na Idadi ya Wakunga Wazinduliwa

  Kaimu Katibu Tawala mkoani Mwanza, Projestus Rubanzibwa, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza, kwenye kikao cha Utambulisho wa Mradi wa kuongeza Ujuzi na Idadi ya Wakunga katika maeneo ya Vijijini katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kanda ya Magharibi, kilichofanyika hii leo Jijini Mwanza. Amesisitiza kwamba Wakuu wa Vyuo vya vya Ukunga nchini wanao wajibu …

Hospitali zatakiwa kuwalinda wapokea kumbukumbu na maambukizi

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bi. Ummy Mwalimu ameziagiza hospitali mbalimbali nchini kuhakikisha zinachukua tahadhari za kuwalinda wafanyakazi wake kitengo cha kumbukumbu katika mazingira ya kupata maambukizi hasa wanapokuwa kazini wakitimiza majukumu yao. Waziri, Mwalimu ametoa maagizo hayo kupitia hotuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi wa Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya kutoka …

Wizara ya Afya Kushirikiana na Taasisi ya Millen Magese Kukabili ‘Endometriosis’

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imesema kuwa ipo tayari kushirikiana na wadau mbalimbali akiwemo Mwanadada Millen Magese na Taasisi yake katika mapambano ya ugonjwa na athari za Endometriosis ambao unawapata wanawake wengi hapa nchini. Kauli hiyo imetolewa mapema leo Machi 30.2016 na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, …

Wizara ya Afya Yaanzisha Kituo cha Kuratibu Matukio ya Sumu

Na Mwanahamisi Matasi – Maelezo WIRAZA ya Afya na Ustawi wa Jamii imeanzisha kituo cha kuratibu matukio ya sumu nchini kilichopo katika maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali. Hayo yamesemwa na Mratibu wa Kituo cha Kuratibu Matukio ya Sumu Nchini Bw. Yohana Mshasi alipokuwa anazungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam na kutoa Elimu ya matumizi na …

Dk. Hamisi Kigwangala Ashtukia Mchezo ‘Mbaya’ Hospitali Binafsi

Na Magreth Kinabo- MAELEZO SERIKALI imepiga marufuku tabia ya baadhi ya hospitali au taasisi binafsi za afya kuwapima wagonjwa wanaotoka hospitali za Serikali vipimo ambavyo hawakuagizwa kuvipima na madaktari kutoka hospitali hizo kwani kufanya hivyo ni kuiongezea Serikali gharama zisizo za lazima. Tamko hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangala …