Kenya Wavamia Kambi ya Al-Shabaab, Waua Wapiganaji 100

MAKAMO wa Rais wa Kenya, William Ruto, amesema kuwa askari wa usalama wa Kenya wamewaandama wapiganaji wa Al-Shabaab hadi kwenye kambi yao nchini Somalia, baada ya shambulio dhidi ya basi Kaskazini – Mashariki mwa Kenya hapo jana ambapo raia 28 wa Kenya waliuliwa. Ruto alisema wapiganaji zaidi ya 100 wa kundi la Al-Shabaab waliuliwa katika operesheni mbili tofauti zilizofanywa na …