Waziri Mkuu Aagiza Kufutwa Umiliki wa Mashamba Makubwa 11 Ngara

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza kufutwa mara moja umiliki wa mashamba makubwa 11 yenye ukubwa wa ekari 7,700 kwenye vijiji vya Kasharazi na Rwakalemera wilayani Ngara Kagera, ambayo hayana hati na yametelekezwa. Ametoa agizo hilo Machi 16, 2016 wakati akizungumza na wakazi wa vijiji vya Kasulo na Rwakalemera katika kata ya Kasulo wilayani Ngara akiwa njiani kuelekea Mkoa wa Geita. …

Waziri Mkuu Majaliwa Ateta na Mabalozi Ofisini Kwake

WAZIRI Mkuu Kasim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na mabalozi watatu kutoka nchi za Uturuki, Ireland na Uswisi pamoja na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa hapa nchini. Akizungumza kwa nyakati tofauti na mabalozi hao Februari 23, 2016, ofisini kwake, Magogoni jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu aliwashukuru mabalozi hao kwa kuja kujitambulisha rasmi na kwa pongezi walizokuja kumpatia na …

Waziri Mkuu Kukamilisha Darala la Mto Mbwemkuru

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema darala la Mto Mbwemkuru lililoko katika barabara ya kutoka Chikwale hadi Liwale litakamilika kwa sababu ni kiungo muhimu kwa wakazi wa eneo hilo. Ametoa ahadi hiyo wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Nangurugai katika kata ya Mbwemkuru wilayani Ruangwa, mkoani Lindi ambako alikwenda kuwashukuru kwa kumchagua kuwa mbunge wao. Waziri Mkuu alikuwa akijibu hoja …