Watoto Wanaonyonya Muda Mrefu Wanaakili na Uwezo

WAKATI hivi sasa wazazi wengi hawapendi kuwanyonyesha watoto wao kwa muda mrefu huku wakiwa na madai na sababu tofauti, utafiti uliofanyika nchini Brazil hivi karibuni umebaini kuwa watoto wanaonyonya kwa muda mrefu wanakuwa na akili zaidi, wasomi, na wenye uwezo kifedha wanapokuwa watu wazima. Ripoti ya utafiti huo iliyochapishwa katika jarida la afya la Lancet Global Health unafuatilia makuzi ya …

Nafasi ya Vyombo vya Habari Kuzuia Ukatili Dhidi ya Watoto

WIZARA ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa ushirikiano na UNICEF wameandaa warsha ya siku tatu inayohusu nafasi ya vyombo vya habari katika kuzuia ukatili dhidi ya watoto nchini Tanzania. Warsha hiyo inayofanyika mjini Moshi inashirikisha wawakilishi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Wawakilishi kutoka Mkoa wa Kilimanjaro, Wawakilishi kutoka wilaya za Hai na Moshi Manispaa, …

Ulemavu wa Kuzaliwa Tatizo Kubwa kwa Watoto Duniani

WATOTO huchukuliwa kama taifa la kesho duniani kote hivyo basi kuwapatia huduma ya afya sahihi lazima ipewe kipaumbele . Mahitaji ya afya ya watoto ni ya kipekee sana, na ya tofauti sana ukilinganisha na watu wazima kwahiyo yanahitaji bidii sana. Mara kwa mara kumekuwepo matukio kadhaa ya kuzaliwa kabla wa wakati, uzito mdogo wa kuzaliwa, mtoto kuzaliwa na kisukari, pumu, …

Taasisi ya Flaviana Matata Yasaidia Watoto 3000

TAASISI ya Flaviana Matata (FMF) ya Mwanamitindo Flaviana Matata aishie New York, Nchini Marekani.   Mwaka jana ilisaidia watoto 3000 kwa kuwapa vifaa vya kujifunzia. Mwaka huu itaendelea kuwasaidia Watoto hao hao wakati inaangalia namna ya kutatua matatizo mengine yanayozikabili Shule hizo ili kuboresha elimu nchini. Yakiwemo mavazi, majengo na hata vyakula vya shule kwa shule za pembezoni Zoezi litaendelea …

Watoto 130,000 Tanzania Wanaishi na VVU

Na Johary Kachwamba – MAELEZO TAKWIMU zinaonesha kwamba watoto 130,000 wana maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI (VVU) kati ya hao 39,317 wamefikiwa na kupatiwa huduma ya dawa za kupunguza makali ya virusi hivyo. Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Pindi Chana wakati akifungua kongamano la nne la kitaifa la VVU na …