Waziri Nape Awasimamisha Kazi Watendaji wa TBC

Na Frank Shija, WHUSM WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amewasimamisha kazi watumishi wawili wa Shirika la Utangazaji la Taifa TBC kutokana na utendaji usioridhisha. Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za TBC leo jijini Dar es Salaam, Waziri Nape amewataja watumishi waliosimamishwa kazi kuwa ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Matukio Bwana Mbwilo Kitujime …