UN Yaipongeza Tanzania Kuwatwaa Warundi 162,156

UMOJA wa Mataifa (UN) umempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete kwa uamuzi wake wa kutoa uraia wa Tanzania kwa waliokuwa wakimbizi 162,156 wa Burundi. Pongezi hizo za UN zimetolewa Oktoba 16, 2014, na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Eneo la Maziwa Makuu, Balozi Said Djinnit wakati alipokutana na kufanya mazungumzo …