Taasisi ya Taaluma za Wanyamapori Mwanza Yazinduwa Jarida

SERIKALI imeahidi kuendelea kuijengea uwezo Taasisi ya Taaluma za Wanyamapori iliyopo Pasiansi jijini Mwanza, ili kukabiliana na matukio ya ujangili ambayo yametikisa nchi miaka ya karibuni. Akizungumza na wanahabari katika uzinduzi wa Makala Maalumu ya Maadhimisho ya miaka 50 na Jarida Maalum la taasisi hiyo, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi, amesema taasisi hiyo imetoa mchango mkubwa katika kufundisha askari wanyamapori ambao wamesaidia …

Mipango ya Wanajamii ni Muhimu Katika Kusimamia Wanyamapori – UNDP

KIONGOZI wa UNDP aliyeko ziarani nchini Tanzania, Helen Clark, amesema usimamizi wa maliasili unaoshirikisha jamii ni ufumbuzi wa muda mrefu na wenye ufanisi zaidi kwa ujangili wa tembo na biashara haramu ya wanyamapori. Akizungumza na watu kutoka vijiji 21 karibu na Hifadhi ya Taifa Ruaha alijifunza uzoefu wao na changamoto za usimamizi katika uhifadhi wa wanyamapori. ‘Ni wazi,’ alisema, ‘kila …